NA MWANDISHI WETU WIMBO wa Seduce Me wa mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba, ameendelea kubamba katika maeneo mbalimbali, wikiendi iliyopita ukiwachizisha vilivyo wakazi wa Mwanza waliohudhuria tamasha la Tigo Fiesta 2017, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Lakini pia, uhondo wa wimbo huo ulinogeshwa zaidi na wakali wa hip hop, Roma Mkatoliki na Stamina, wanaounda umoja walioupa jina la Rostam, ambao walipanda jukwaani kivingine kwa kila mmoja kuwa na baiskeli yake na kuweka kitu tofauti kwenye wimbo wao wa Huku Ama Kule. Manjonjo hayo yaliyofanywa na Rostam pamoja na uhondo wa Seduce Me, uliufanya Uwanja wa CCM Kirumba kulipuka kwa shangwe kutoka kwa mashabiki wa burudani waliofika uwanjani hapo kupata burudani kutoka kwa sanii wao wakali wa hapa nchini. Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo Tanzania, alikuwa ni msanii wa kufokafoka, Rosa Ree, ambaye alifungua pazia la burudani na kuonyesha jinsi gani anakuja kwa kasi katika muziki pale alipoimba kwa umahiri wa hali ya ...
Comments