TUCTA kumjibu Rais Magufuli – Mtembezi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amekagua ujenzi wa Jengo la Huduma Dharura ya kwenye Hospitali ya Rufaa Temeke ambayo Ujenzi wake unafadhiliwa na Ubalozi wa Japan Nchini Tanzania.

Ujenzi wa Jengo hilo unagharimu kiasi cha Shillingi Million 800 ambazo ni matunda ya jitiada binafsi za RC Makonda baada ya kumtafuta Balozi wa Japan Nchini Tanzania na kumueleza changamoto ya ukosefu wa kitengo cha Huduma za haraka kwenye Hospital za Mkoa ambapo baada ya mazungumzo Balozi alipokea kwa mikono miwili ombi la RC Makonda.

RC Makonda amesema kukamilika kwa jengo hilo itasaidia kupunguza Vifo vitokanavyo na Wagonjwa wanaohitaji huduma ya haraka kuikosa huduma hiyo kwa uharaka.

Amesema jengo hilo ni mahususi kwajili ya wagonjwa wote wanaohitaji huduma ya haraka hususani Majeruhi wa Ajali, Wanaougua Malaria kali ya gafla, Maumivu ya Tumbo, wanaobanwa na Kifu, Wajawazito, Homa kali, ajali ya Moto na Magonjwa yote yanayohitaji huduma ya haraka.

Amebainisha kuwa wagonjwa wanaohitaji huduma ya haraka wanaofikishwa Hospitalini hapo wamekuwa wakipelekwa Hospital ya Muhimbili ambako ni mbali kutoka Temeke hivyo kusababisha wengi wao kupoteza maisha Barabarani.

Aidha Makonda amesema baada ya kumalizika kwa jengo hilo ujenzi wa majengo ya huduma ya haraka utahamia kwenye Hospital ya Amana na Mwananyamala ilikuipungizia mzigo Muhimbili

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Temeke Dr. Aman Malima amesema kwa siku wanapokea wagonjwa kati ya 1,800 -2,000 ambapo kati ya hao 200 ni wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharura hivyo amesema uwepo wa huduma hiyo itasaidia kuokoa maisha.

Amempongeza RC Makonda kwa juhudi zake binafsi za kutafuta wadau waliofanikisha ujenzi wa Jengo hilo.

Nae Mkandarasi wa ujenzi huo Bwana Abdulkadir Msangi amesema ujenzi umefikia 85% ambapo hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi November ujenzi utakuwa umekamilika na jengo kukabidhiwa.

The post RC Makonda akagua ujenzi wa jengo la dharula Hospitali ya Rufaa Temeke appeared first on Mtembezi.

READ MORE

from Habari Za Tanzania
vRead More

Comments

Popular This Week

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

Popular This Month

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya