Rais Magufuli atembelea TAKUKURU na kutoa maagizo kuhusu kesi za rushwa | habari

Share


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 28 Agosti, 2017 alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa TAKUKURU katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

“Kuna mambo mengi ya hovyo yanafanyika, tumehakiki pembejeo za ruzuku na kubaini madai ya Shilingi Bilioni 48 ni hewa, tumebaini wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, tumebaini kaya masikini hewa 56,000 zilizopaswa kupata fedha TASAF, tumebaini wanafunzi hewa 5,850 waliotakiwa kupata mkopo, kuna vichwa vya treni 11 vimeletwa bila kuwepo mkataba na mengine mengi, haya yote yanafanyika kwa rushwa, nataka kuwaona mnachukua hatua stahiki” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amesema ana imani na TAKUKURU na amewataka wafanyakazi wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu mkubwa na kwamba Serikali itafanyia kazi changamoto zinazowakabili.

Katika mkutano huo Mhe. Rais Magufuli amepokea masuala mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa TAKUKURU na amewaahidi kuwa Serikali itayafanyia kazi ili kuboresha maslahi yao na mazingira ya kazi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Katibu Mkuu Dkt. Laurian Ndumbaro na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi na wataalamu wanaosimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stieglers’ Gorge Hydropower Project), ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) na ujenzi wa barabara mbalimbali nchini, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika Mkutano huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Matogolo Kalemani ametoa taarifa ya maandalizi ya awali ya kuanza kwa ujenzi wa mradi wa umeme wa Stiegler’ Gorge na kwamba zabuni ya kuanza kwa ujenzi huo itatangazwa tarehe 30 Agosti, 2017.

Mhe. Rais Magufuli amesema fedha za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa utakaozalisha Megawatts 2,100 zitakazoingizwa katika gridi ya Taifa zipo.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiingia  Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Upanga jijini Dar es salaam Agosti 28, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Upanga jijini Dar es salaam Agosti 28, 2017 .  Wengine ni  Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora)Mhe. Angela Kairuki,  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dr. Laurean Ndumbaro, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlowola, na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAKUKURU Bw. Alex Mfungo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa anaongea na  wafanyakazi wa Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Upanga jijini Dar es salaam 28 Agosti 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Upanga jijini Dar es salaam Agosti 28,2017.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

28 Agosti, 2017

READ MORE

Share



from AutoMedia Tanzania
via Read More

Comments

Popular This Week

JOHN HECHE:WATU HAWAKO SALAMA NCHI HII, NI BAADA YA MDOGO WAKE KUUAWA NA POLISI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

DIWANI WA CCM APOTEZA MAISHA KWA AJALI ASUBUHI YA LEO. | Darmpya

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

AUDIO | DJ Mwanga

MAHAKAMA NCHINI ZAMBIA YAAGIZA MWANAMUZIKI KOFII OLOMIDE KUKAMATWA. | Darmpya

RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO | noreply@blogger.com (Muhidin Sufiani)

MAVUNDE AAGIZA KUFANYIKA UCHUNGUZI, KUBAINI FEDHA ZA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA VIJANA ZILIPOKWENDA | Darmpya

VIDEO | DJ Mwanga

Popular This Month

AUDIO | DJ Mwanga

JOHN HECHE:WATU HAWAKO SALAMA NCHI HII, NI BAADA YA MDOGO WAKE KUUAWA NA POLISI | Darmpya

DIWANI WA CCM APOTEZA MAISHA KWA AJALI ASUBUHI YA LEO. | Darmpya

House Victimz – Victimized Vol.1 Album | AutoMedia Tanzania

MBUNGE KUBENEA AMUUMBUA RC MAKONDA , | Darmpya

SASA ZAMU YA WAKUU WA WILAYA, RAIS MAGUFULI AMTUMBUA DC KAHAMA | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

MAHAKAMA NCHINI ZAMBIA YAAGIZA MWANAMUZIKI KOFII OLOMIDE KUKAMATWA. | Darmpya

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya