Mkojo waonesha Masogange anatumia dawa za kulevya | Emmanuel Shilatu

Share


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea taarifa ya mkemia wa serikali iliyoonesha kwamba sampuli ya mkojo wa Video Queen, Agnes Gerald “Masogange” una chembechembe za dawa za kulevya.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema leo kwamba pingamizi la upande wa utetezi kuwa fomu zilizopelekwa kwa mkemia hazikufata sheria limetupiliwa mbali na mahakama imepokea taarifa hiyo ambayo itatumika kama ushahidi.

Amesema shahidi wa kwanza ambaye ni Elia Mulima anahaki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti mahakamani. Pia amesema Polisi walipeleka maombi kwa mkemia wa serikali na kwamba ni wazi mshitakiwa alienda kwa mkemia na askari wawili na kumpatia kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo.

Mpelelezi kutoka Ofisi ya Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, WP Judith ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa alishuhudia Masogange akitoa sampuli ya mkojo kwa kuwa alisimama mlangoni.

Amedai kuwa alipewa chupa ya plastiki yenye namba ya maabara 446/2017 na kumuelekeza Masogange jinsi ya kufanya ambapo alipata sampuli ya mkojo huo. Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, shahidi huyo alidai kuwa Februari 15, mwaka huu aliitwa na Kaimu Mkuu wa Upelelezi, Ramadhan Kingai amchukue mshitakiwa Masogange na kumpeleka kwa Mkemia wa Serikali.

Amedai baada ya kuchukua aliongozana na Askari Polisi, Sospeter kwenda kwa mkemia na kwamba saa 7 mchana walifika. “Lengo la kumpeleka kwa mkemia ni kupimwa sampuli ya mkojo kwa kuwa alituhumiwa kwa kutumia au kusafirisha dawa za kulevya,” alidai Judith.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Reuben Simwanza alimtaka shahidi huyo kueleza alikabidhiwa na nani chupa na kwamba mkojo ulikuwa na rangi ambapo shahidi huyo alieleza kuwa ulikuwa na rangi ya njano mpauko. Hakimu Wilbard Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 31, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.


READ MORE

Share



from AutoMedia Tanzania
via Read More

Comments

Popular This Week

JOHN HECHE:WATU HAWAKO SALAMA NCHI HII, NI BAADA YA MDOGO WAKE KUUAWA NA POLISI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

DIWANI WA CCM APOTEZA MAISHA KWA AJALI ASUBUHI YA LEO. | Darmpya

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

AUDIO | DJ Mwanga

MAHAKAMA NCHINI ZAMBIA YAAGIZA MWANAMUZIKI KOFII OLOMIDE KUKAMATWA. | Darmpya

RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO | noreply@blogger.com (Muhidin Sufiani)

MAVUNDE AAGIZA KUFANYIKA UCHUNGUZI, KUBAINI FEDHA ZA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA VIJANA ZILIPOKWENDA | Darmpya

VIDEO | DJ Mwanga

Popular This Month

AUDIO | DJ Mwanga

JOHN HECHE:WATU HAWAKO SALAMA NCHI HII, NI BAADA YA MDOGO WAKE KUUAWA NA POLISI | Darmpya

DIWANI WA CCM APOTEZA MAISHA KWA AJALI ASUBUHI YA LEO. | Darmpya

House Victimz – Victimized Vol.1 Album | AutoMedia Tanzania

MBUNGE KUBENEA AMUUMBUA RC MAKONDA , | Darmpya

SASA ZAMU YA WAKUU WA WILAYA, RAIS MAGUFULI AMTUMBUA DC KAHAMA | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

MAHAKAMA NCHINI ZAMBIA YAAGIZA MWANAMUZIKI KOFII OLOMIDE KUKAMATWA. | Darmpya

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya