Bulaya Aruhusiwa Kutoka Muhimbili | Bigie

Share


Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa takribani wiki moja.

Bulaya alikimbizwa Muhimbili kutoka tarime mkoani Mara baada ya kupata tatizo la kupumua baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya kituo cha polisi mjini Tarime. Alikuwa amelazwa wodi namba 18 katika jengo la Sewahaji akipatiwa matibabu.

Mbunge huyo wa Chadema, leo Agosti 28 ameruhusiwa kutoka hospitali na amewashukuru madaktari wa Muhimbili kwa kumpatia matibabu ya kina.

Amesema afya yake imetengemaa lakini amepewa maelekezo kadhaa.

“Kwanza nitapumzika kwa siku 10, hivyo ndivyo nilivyoagizwa na nitatakiwa kurudi tena hospitalini kwa ajili ya kuangaliwa afya yangu zaidi. Kwa sasa nitapumzika kabla ya kurudi jimboni kuendelea  na shughuli za maendeleo,” amesema Bulaya.

Bulaya aliwekwa rumande Agosti 18 baada ya kukamatwa na polisi akidaiwa kuingia jimbo la Tarime kufanya shughuli za kisiasa kwa kutoa msaada wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi kwa mwaliko wa mbunge mwenzake Esther Matiko.

READ MORE

Share



from AutoMedia Tanzania
via Read More

Comments

Popular This Week

HISTORIA YA WANGONI NA LILIPOTOKA JINA LA SONGEA | noreply@blogger.com (Lewis Mbonde)

MKEMIA MKUU: ‘Wanafunzi wanaoenda vyuoni wapimwe matumizi ya dawa za kulevya’ | Millardayo

Sina Beef Na Mange Kimambi Ananipenda Na Ananikubali : Wolper – Jicho La Uswazi | Mcinika Wa Lamar

KESI YA KUPINGA KUONDOLEWA CHANEL ZA NDANI KWENYE VISIMBUZI KUTAJWA OCTOBA 18 | Darmpya

MAMILIONI YA MFUKO WA JIMBO NYAMAGANA YAMWAGWA SOKO LA MLANGO MMOJA. | Darmpya

Kesi ya Aveva, Kaburu TAKUKURU yakiri upelelezi haujakamilika | Millardayo

Popular This Month

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BILL GATES NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI | MICHUZI BLOG

HISTORIA YA WANGONI NA LILIPOTOKA JINA LA SONGEA | noreply@blogger.com (Lewis Mbonde)

Dubai yazindua jengo refu zaidi duniani lenye ghorofa 75 | Darmpya

Birdman wa CashMoney anakuja Tanzania | Millardayo

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya