JPM atengua uteuzi wa mkurugenzi wa Mkinga
Dar es Salaam. Siku moja baada ya kushtakiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga, Emmanuel Mkumbo, Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi huyo kuanzia leo Jumanne.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa uteuzi wa takayejaza nafasi ya Mkumbo utafanywa baadaye.
Mkumbo alishtakiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwa makosa mawili ambayo ni la kudaiwa kutishia kuua na makosa ya usalama barabarani.
Comments