Posts

Showing posts with the label Habari

RC SHINYANGA ATOA MABATI 171 KWA SHULE TATU WILANI KISHAPU

Image
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ametoa msaada wa mabati 171 kwa shule za msingi tatu wilayani Kishapu mkoani hapa kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa pindi yatakapokamilika ujenzi wake. Telack alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilobi, kata ya Mwaweja wilayani hapa alipofanya ziara ya kikazi ambapo pia alitumia nafasi hiyo kusikiliza kero zao. Katika msaada huo jumla ya shule tatu za Nyenze iliyopo kata ya Idukilo, Mwasubi kata ya Bunambiyu na Ilobi kwenye kata ya Mwaweja zitanufaika na msaada huo wa mabati 57 kila moja. Akiwa katika ziara hiyo ya kikazi wilayani hapa, Telack aliagiza wazazi wote kijijini hapo wawapeleke watoto wao na kuwaandikisha shuleni ambapo alisisitiza umuhimu wa elimu kwao. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilobi kata ya Mwaweja alipofanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese. Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalam...

VINGUNGUTI WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI

Image
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wazazi kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa kuchangia maendeleo ya elimu. Kumbilamoto amesema hayo katika mkutano wake na wazazi wa shule  ya Msingi Miembeni kata ya Vingunguti . “lazima niwambie ukweli, hili suala la elimu bure limetusaidia sana katika kata yetu ya vingunguti, hivyo ni vyema kila mtu akawa na wajibu wa kuchangia angalau kidogo katika maendeleo ya elimu kama sadaka ili watoto wetu waishi katika mazingira mazuri” amesema Kumbilmoto. Kumbilamoto ametolea mfano uwepo wa mabembea katika shule za msingi katika nchi za falme za kiarabu, ambako alikuwa mapumzikoni hivi karibuni ,amesema shule za vingunguti lazima ziwe na bembea kama za uarabuni. Aidha amepata kuchangia ndoo mbili za rangi na makopo manne kwa ajili ya kupakwa katika darasa la kwanza . Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Idaya Ndevu mbili alimshukuru Meya huyo kwa msaada wake na kumuomba aendelee na moyo huo h...

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA UBUNGO LAPITISHA KWA 100% BAJETI YA ZAIDI YA BILIONI MIA MOJA

Image
Baraza la madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam kwa kauli moja limepitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa kuungwa mkono na madiwani wote waliozuru katika mkutano maalumu wa baraza hilo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kaimu Afisa habari na Uhusiano wa Manispaa hiyo Bi Maria Makombe imeeleza kuwa Katika mpango huo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inakadiria kukusanya/kupokea kiasi cha Tshs 128,611,616,805.100 ambazo zimeelekezwa katika matumizi ya mishahara, utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na matumizi mengineyo. Fedha hizo zitatokana na makusanyo ya ndani ya Halmashauri, Ruzuku kutoka serikali kuu, Michango ya wananchi na wahisani wa Maendeleo.Aidha Halmashauri inatarajia kupokea kiasi cha Tshs 4,233,546,143.00 kutoka TAMISEMI kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara (Road Fund). Katika fedha hizo chanzo cha makusanyo ya ndani ni Tshs 24,006,600,000.00 ambayo ni ...

SHULE YA MSINGI YA TUMAINI AMBAYO IPO MAENEO YA KIWANJA CHA NDEGE CHA BUKOBA SASA KUJENGWA ENEO JINGINE, KUTOKANA NA USALAMA.

Image
  Baadhi    ya madarasa ya shule ya msingi Tumaini iliyopo kata ya Kashai, wilaya ya Bukoba Mjini ambayo wanafunzi watahamishwa kwa kujenegwa shule nyingene katika eneo la  mtaa wa Mafumbo, kata ya Kashai  kutokana na usalama baada ya kuwa karibu na eneo la Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.   Baadhi ya majengo mapya ya madarasa ya shule mpya ya msingi ya Tumaini, yaliyopo mtaa wa Mafumbo, kata ya Kashai yakiwa kwenye hatua ya mwisho ya ujenzi wake. Shule hii inamadarasa 24 ya kuanzia darasa la kwanza hadi la Saba, na madarasa matatu kati ya hayo ni ya watoto wenye mahitaji maalumu.   Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Rwambaizi ya Karagwe wakiwa    kwenye kiwanja cha ndege cha Bukoba, katika ziara ya mafunzo.   Abiria wakiwasilisha taarifa zao ikiwemo na ukaguzi wa tiketi, kabla ya kupanda ndege ya Auric    wakitokea kwenye kiwanja cha ndege cha Bukoba wakielekea Mwanza. Msimamizi wa Kitengo cha Usalama, Bi. ...

ZIARA YA KATIBU WA KAMATI MAALUM YA NEC IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA,MHANDISI HAMAD MASAUNI VISIWANI ZANZIBAR

Image
 K atibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na    Uhusiano wa Kimataifa    Zanzibar , Mhandisi Hamad Masauni,    akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji    hufanyika hapo ambapo ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria .   Katibu wa Kamati Maalum ya NEC    Idara ya Siasa na    Uhusiano wa Kimataifa    Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jeraha la mmoja wa wananchi wa eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi, ambaye wiki chache zilizopita alijeruhiwa na mapanga na watu wanaofanya matendo ya uhalifu katika eneo hilo.   Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma, akizungumza na vyombo vya habari juu ya ha...

DK.SHEIN AONDOKA NCHINI LEO, AENDA INDONESIA

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi wakuu wa Vikosi vya Ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo wakati alipokuwa akiondoka Nchini kueleke Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),katika safari hiyo akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Mawaziri na Viongozi mbali mbali Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM na Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka Nchini leo kueleke Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA). Rais wa Zanzi...

MAMA SAMIA MGENI RASMI UKARIBISHO WA VIONGOZI DODOMA.

Image
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla maalumu ya kuwakaribisha viongozi wa Serikali itakayofanyika Machi 5 mwaka huu mkoani Dodoma. Hafla hiyo imeandaliwa na Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Dodoma na itafanyika mkoani humo katika viwanja vya Nyerere (Nyerere Square) kuanzia saa 8 kamili mchana. Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Jeremia Mwakyoma ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya ujio wa viongozi hao katika Mkoa huo. Mwakyoma amesema viongozi wa Serikali kuhamia katika Makao Makuu ya Nchi ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano hivyo Mkoa utawakaribisha rasmi Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara waliohamia kutoka Jijini Dar es Salaam. “Tukio la viongozi wa Wizara kuhamia Makao Makuu Dodoma ni la kihistoria ndio maana uongozi wa Serikali ya Mkoa umeona ni vema kuweka utaratibu rasmi wa kuwaka...

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA GATI NAMBA 2 KATIKA BANDARI YA MTWARA PIA AFUNGUA JENGO LA KITUO CHA KIBIASHARA CHA BENKI YA NMB MTWARA

Image
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika Ujenzi wa  Gati namba mbili litakayojengwa katika Bandari ya Mtwara.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  Mhandisi Deusdedit Kakoko kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisikiliza maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  Mhandisi Deusdedit Kakoko kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufu...

Utafiti: Tembo ndio mnyama anayelala kwa muda mfupi zaidi duniani

Image
Wanasayansi waliowafuatilia ndovu wawili nchini Botswana wamebaini kuwa wanyama hao hulala muda mfupi zaidi ya mnyama mwengine yeyote duniani. Ndovu hulala kwa saa mbili pekee hususan nyakati za usiku. Wakiwa katika hifadhi, ndovu hulala kati ya masaa manne hadi sita kwa siku. Mbwa achaguliwa tena kuwa meya Minnesota, Marekani Wanyama waliowahi kushinda nyadhifa uchaguzini Ndovu hao wote wakiwa viongozi wa familia zao mara nyengine husalia macho kwa siku kadhaa na huonekana wakifunga macho ama kuota mara moja kila siku tatu ama hata nne. Haijulikani kwa nini wanyama hao walio na uwezo mkubwa wa kukumbuka vitu wanaweza kuishi kwa kulala kwa muda mfupi licha ya usingizi kuwa na muhimu mkubwa katika ubongo .

Afcon 2017: Ivory Coast uso kwa uso na kocha wake wa zamani Herve Renard

Image
Image caption Morocco and Ivory Coast watachuana mara tatu ndani ya miezi michache ijayo Timu ya taifa ya Ivory Coast itapambana na kocha wake wa zamani Herve Renard baada ya kupangiwa katika kundi moja na Morocco katika michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika. Renard aliiongoza Ivory Coast katika fainali za kombe hilo mwaka 2015 na sasa anakwenda tena Gabon akiwa na kikosi cha nchi tofauti. Gabon watafungua mashindano hayo Januari 14, huku mchezo wa fainali ukipangwa kuwa Februari 5. Muonekano wa timu na makundi AFCON 2017 KUNDI  A Gabon Burkina Faso Cameroon Guinea Bissau KUNDI B Algeria Tunisia Senegal Zimbabwe KUNDI C Ivory Coast DR Kongo Morocco Togo GROUP D Ghana Mali Misri Uganda

Popular This Month

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya