Posts

Showing posts with the label mpya

Zitto awasilisha muswada mafuta, gesi ya Zanzibar

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amewasilisha rasmi muswada binafsi wa Sheria ya Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu mafuta na gesi ya Zanzibar. Zitto amesema amefanya hivyo katika kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia wa  ACT Wazalendo uliofanyika Oktoba 2016, baada ya mjadala wa mada kuhusu Zanzibar na Katiba ya Muungano. Zitto alisema hoja hiyo inakuwa muhimu kwa sasa kwa sababu ya kunusuru uvunjwaji wa Katiba ulio wazi. “Kusubiri Katiba Mpya hakuhalalishi iliyopo kuvunjwa. Kwa kuwa mabadiliko ya Katiba Mpya yamekwama bila ya kauli ya Serikali kujua lini mchakato utaendelea, hii hoja yetu ni ya lazima kwa sasa katika kuhalalisha hatua ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kutunga sheria inayohusiana na mafuta na gesi asilia,” alisema Zitto.

Panya Road wa Mbagala watiwa mbaroni

Image
Dar es Salaam.  Jeshi la polisi mkoa wa Temeke limewakamata watu zaidi ya 15 wanaodaiwa kuwa ni Panya Road waliovamia na kuwapora  watu waliokuwa wakitoka kwenye tamasha la kuinua vipaji lililoandaliwa na redio ya  Clouds. Wahalifu hao wanadaiwa kufanya uhalifu rmaeneo ya Sabasaba, Temeke, huku wakiwa na silaha za kijadi ikiwamo mapanga maeneo ya Sabasaba. Kamanda wa polisi mkoa huo,Gilles Muroto alisema Oktoba 15 saa 11 jioni  liliandaliwa  tamasha la kuinua vipaji na Clous FM ambapo vijana hao walishiriki na baadaye kufanya uhalifu huo. Alisema baada ya tamasha hilo kwisha watuhumiwa hao wanaodaiwa kuwa zaidi ya 50 waliingia mtaani huku na kuelekea eneo la sabasaba wakiwa na mapanga,visu,bisibisi kwa ajili ya kufanyia uhalifu. Muroto alisema wakati wakielekea eneo hilo ndipo wananchi waliwadhibiti na kuwakamata vijana sita kati ya hao mmoja alifariki wakati akipelekwa hospitali,wawili wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya temeke na watatu walitoa ushirikiano ...

Upepo waezua shule, watoto sita wajeruhiwa

Image
Picha na Phinias Bashaya,  Mwananchi Missenyi.  Upepo mkali umeezua vyumba sita vya madarasa karika Shule ya Msingi Byamutemba wilayani hapa mkoani Kagera na kujeruhi wanafunzi sita. Kutokana na tukio hilo lililoathiri pia nyumba za wakazi wa eneo hilo ambazo idadi yake haijafahamika, Serikali imeifunga kwa muda usiojulikana shule hiyo, ikisubiri kuijenga baada ya taratibu kukamilika. Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Limbe Mourice amesema majeruhi hao wamelazwa katika Kituo cha Afya Bunazi. Kwa siku za karibuni Mkoa wa Kagera umekumbwa na mabalaa likiwamo tetemeko la ardhi liliua watu 17 na kusababisha nyumba zaidi ya 3,000 kuanguka na hadi sasa nyingi hazijajengwa.

JPM atengua uteuzi wa mkurugenzi wa Mkinga

Image
Dar es Salaam.  Siku moja baada ya kushtakiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga, Emmanuel Mkumbo, Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi huyo kuanzia leo Jumanne. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa uteuzi wa takayejaza nafasi ya Mkumbo utafanywa baadaye. Mkumbo alishtakiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwa makosa mawili ambayo ni la kudaiwa kutishia kuua na makosa ya usalama barabarani.

Mourinho: Tulidhibiti mechi na kuwanyamazisha mashabiki wao

Image
Image caption Mkufunzi wa man United Jose Mourinho Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa timu yake ilidhibiti mpira pamoja na kufunga midomo ya mashabiki wa Anfield. Akihojiwa baada ya mechi hiyo iliotoka sare ya bila kwa bila,Mourinho amesema kuwa ijapokuwa hakutarajia matokeo hayo timu yake ilifanikiwa kuizuia Liverpool kwa kudhibiti mchezo kwa muda mrefu. ''Tulifanikiwa kudhibiti kelele za mashabiki wa Anfield pamoja na mchezo wa timu yao''. Mourinho amesema kuwa ijapokuwa wengi walidhani watashindwa timu yake iliodhibiti mpira na kuwapatia kibarua kigumu wapinzani wao. Hatahivyo mkufunzi huyo amekiri kwamba safu ya ushambuliaji ya Manchester United haikuwa imara wakati wa mechi hiyo. Image copyright GETTY IMAGES Image caption Man United ikichuana na Liverpool katika uga wa Anfield .Mechi hiyo ilikamilika katika sare ya bila kwa bila ''Hatahivyo nadhani hatukuimarika vilivyo katika safu ya mbele.Nashukuru kwamba pointi yetu moja il...

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Image
Image caption Jeshi la Iraq, likiupigania mji wa Mosul Majeshi ya serikali ya Iraq na Wapiganaji wa Kikurd wamepiga hatua muhimu katika siku yao ya kwanza ya mashambulizi makali dhidi ya kundi la Islamic State katika mji wa Mosul. Ndege za kivita za Marekani zimeunga mkono kampeni hiyo, iliyoanza jana. Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema malengo ya siku ya kwanza yaliyowekwa yalitimia, licha ya kutokea makabiliano ya hapa na pale na wapiganaji hao wenye itikadi kali. Katika hatua nyingine Umoja wa Mataifa umesema unaharakisha kukamilisha kambi za dharura kwa ajili ya kuwahifadhi raia, ambao wanaweza kuyakimbia makaazi yao kutokana na mapigano.

Wanawake wawili wamshtumu Donald Trump kuwapapasa kimapenzi

Image
na RFI Donald Trump, akiwa na bango mkononi lililoandikwa "wanawake pamoja na Trump", katika mkutano wa hadhara mjini Lakeland, Oktoba 12, 2016. REUTERS Gazeti la New York Times limechapishwa Alhamisi hii asubuhi ushahidi wa wanawake wawili ambao wanasema kuwa walishambuliwa kingono na Donald Trump. Mgombea urais wa chama cha Republican tayari ameumbuka na video ya mwaka 2005 ambapo anazungumzia mambo ya uasherati. Watu wengi nchini Marekani wanajiuliza kwa nini Donald Trump hakusikia ushauri mwema kutoka kwa wajumbe wa chama cha Republican kwa ajili yake, wale waliomshauri kufunga ukurasa wa kauli zake za uasharati na hivyo kuomba tu radhi kwa yale yaliyotokea? Mgombea huyo aliamua kulipiza kisasi, na kutoa wito katika mjadala wa mwisho kwa makahaba wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton katika mwaka mwaka 1990. Matokeo ya kauli ya Bw Trump yameanza kujitokea. Wanawake leo wanamshtumu mgombea urais wa chama cha Republican aliwapapasa kimapenzi pila idhni yao. Katika gaze...

Michelle Obama amkosoa Donald Trump.

Michelle Obama, mke wa rais wa Marekani, Barack Obama, amekosoa kauli ya Donald Trump ambayo amesema imewadhalalisha wanawake. Mgombea wa chama cha Republican anayetuhumiwa kuwanyanyasa kijinsia wanawake amesema analengwa na 'uongo wenye aibu' uliopangwa na mshindani wake kutoka chama cha Denocrat kupitia vyombo vya habari kwa minajili ya kumuangusha kisiasa. "Katika chama chohote kile unachotetea, sawa na Democrat, Republican au mgombea binafsi, hakuna mwanamke anastahili kudhalilishwa kwa namna hii," amesema mke wa Rais wa Marekani Barack Obama, katika hotuba aliyoitoa Alhamisi wiki hii. Michelle Obama ametoa hotuba hiyo kufuatia kauli chafu na yenye kejeli inayowadhalilisha wanawake iliyotolewa na Donald Trump mwaka 2005. Tangu maeneo yake hayo yawekwe wazi, Bw Trump ameshindwa kutuliza hali ya sintofahamu iliyosababishwa na kauli yake hiyo ndani ya chama chake pamoja na katika jamii nzima hasa wanawake nchini Marekani. Hali hii ilianza kuwa mbaya zaidi tangu Jumat...

Wasiwasi waendelea Duniani kuhusu simu hatari ya Galaxy note 7

Image
Samsung kuwatumia wateja wake walioko Marekani makasha yanayoweza kustahimili moto, kuweka Note 7 wanazorejesha Kampuni ya vifaa vya eletroniki ya Samsung imetangaza kuwatumia wateja wake walioko Marekani makasha yanayoweza kustahimili moto, kama tahadhari dhidi ya uwezekano wa kutokea moto au kulipuka kwa simu zake aiana ya Galaxy Note 7 walizorejesha kwa wauzaji simu hizo nchini humo. Makasha hayo hasa yanatolewa kwa wateja walionunua simu hizo katika tovuti yake ya Samsung.com. Walio na simu hiyo aina ya Galazy Note 7 pia wameshauriwa kutembelea tovuti ya Samsung kufahamu maelekezo ya kuzirejesha. Kampuni hiyo ya Samsung imetangaza kusitisha utengenezaji wa simu hiyo ya Galazy note 7 miezi miwili baada ya kuizindua upya, baada ya kurekebishwa mara ya pili, kufuatia ripoti kadhaa za simu hiyo kushika moto.Samsung sasa italazimika kupokea zaidi ya Galazy Note 7 million 1.5 ilizokuwa tayari imeuza au kutoa kama simu mbadala. Nyingi ya simu hizo ziliuzwa Marekani na Korea Kusini. Hata i...

MWALIMU ASAKWA NA POLISI KILIMANJARO KWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

Image
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa By Fina Lyimo na Bahati Chume, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz Hai . Polisi mkoani Kilimanjaro  inamsaka mwalimu wa Shule ya Sekondari Lemira wilayani hapa anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne na kukimbilia kusikojulikana. Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa mzazi wa mwanafuzi huyo na mkuu wa shule wanashikiliwa ili kusaidia kupatikana kwa mawlimu huyo. Amesema mzazi aligundua kuwa mwanaye ana ujauzito wa miezi mitano na alipomuuliza alimwambia mhusika ni mwalimu wake. “Mzazi wa mtoto alimfuata mwalimu huyo aliyekubali kuwa ujauzito ni wake na kwamba atamuoa. Alimtaka aweke kwenye maandishi kuwa ujauzito ni wake na atamuoa,” alisema Mutafungwa. Amesema mwalimu huyo alikubali na kuandika kuwa atamuoa mwanafuzi atakapojifungua na kwamba, mkuu wa wilaya alipopata habari hizo alizifuatilia ili kujua sababu. Alisema alipoitwa kwa mkuu wa wilaya, mwalimu huyo a...

Ngassa afunga Goli lake la kwanza akicheza Fanja FC ya Oman

Image
MICHEZO Winga wa kimataifa wa  Tanzania anayecheza soka katika klabu ya  Fanja FC ya  Oman   Mrisho Ngassa   amefanikiwa kuanza maisha yake mapya ya soka katika klabu hiyo kwa kufunga goli akicheza mchezo wake wa kwanza toka ajiunge na klabu hiyo. Ngassa  ambaye amejiunga na  Fanja FC akiungana na aliyekuwa mshambuliaji wa Simba   Danny Lyanga  amefunga goli katika mchezo dhidi ya  Al-Nahda , mchezo ambao umemalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2.

RATIBA LIGI KUU YA UINGEREZA OCTOBA 2016

SAT 15 OCT Chelsea V Leicester 12:30 kick off Arsenal V Swansea 15:00 kick off Bournemouth V Hull 15:00 kick off Man City V Everton 15:00 kick off Stoke V Sunderland 15:00 kick off West Brom V Tottenham 15:00 kick off Crystal Palace V West Ham 17:30 kick off SUN 16 OCT Middlesbrough V Watford 13:30 kick off Southampton V Burnley 16:00 kick off MON 17 OCT Liverpool V Man Utd 20:00 kick off SAT 22 OCT Bournemouth V Tottenham 12:30 kick off Arsenal V Middlesbrough 15:00 kick off Burnley V Everton 15:00 kick off Hull V Stoke 15:00 kick off Leicester V Crystal Palace 15:00 kick off Swansea V Watford 15:00 kick off West Ham V Sunderland 15:00 kick off Liverpool V West Brom 17:30 kick off SUN 23 OCT Man City V Southampton 13:30 kick off Chelsea V Man Utd 16:00 kick off SAT 29 OCT Sunderland V Arsenal 12:30 kick off Man Utd V Burnley 15:00 kick off Middlesbrough V Bournemouth 15:00 kick off Tottenham V Leicester 15:00 kick off Watford V Hull 15:00 kick off West Brom V Man City 15:00 kick off C...

Popular This Month

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya