Posts

Showing posts with the label news

FIFA: Argentina bado wababe, Tanzania washuka

Image
Image copyright AFP Image caption Argentina wameendelea kuongoza orodha hiyo ya ubora Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka duniani, ambapo vinara wamesalia kuwa Argentina. Wanafuatwa kwa karibu na mabingwa wa dunia Ujerumani, kisha Brazil wanashika nafasi ya tatu. Ubelgiji imeshuka nafasi mbili hadi nambari nne. Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi. Tanzania sasa inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka nafasi 12. Uganda wamo nambari 72 baada ya kushuka nafasi saba, Kenya wamepanda nafasi sita hadi nambari 85 nao Rwanda wamesalia nambari 107. Ethiopia wamo nafasi ya 126, Malawi 100 na Burundi 138. Nchi ya juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32. Orodha nyingine ya Ubora wa viwango itatolewa Novemba 24. Mataifa 10 bora duniani 1.Argentina 2.Ujerumani 3.Brazil 4.Ubelg...

Akon azuru Liberia kuweka umeme katika shule 2

Image
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Mwanamuziki wa mtindo wa Hip Hop azuru nchini Liberia Mwanamuziki wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Akon yuko ziarani nchini Liberia kuweka umeme wa jua katika shule mbili za msingi katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Ni miongoni mwa miradi yake ya kuwawekea umeme watu milioni 600 katika bara la Afrika. Akon ambaye ni mzaliwa wa Senegal anashirikiana na kampuni ya Bridge International Academies pamoja na ushirikiano na mashirika mengine ya kimatifa kusimamia shule 50 nchini Liberia. Wakati msafara wake wa magari ulipokuwa ukipita katika mji mkuu wa Monrovia,chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi,mwanamuziki huyo alisema kuwa inasikitisha kuona kwamba hakuna umeme katika barabara ya kilomita 50 kutoka uwanja wa ndege.

Akon azuru Liberia kuweka umeme katika shule 2

Image
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Mwanamuziki wa mtindo wa Hip Hop azuru nchini Liberia Mwanamuziki wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Akon yuko ziarani nchini Liberia kuweka umeme wa jua katika shule mbili za msingi katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Ni miongoni mwa miradi yake ya kuwawekea umeme watu milioni 600 katika bara la Afrika. Akon ambaye ni mzaliwa wa Senegal anashirikiana na kampuni ya Bridge International Academies pamoja na ushirikiano na mashirika mengine ya kimatifa kusimamia shule 50 nchini Liberia. Wakati msafara wake wa magari ulipokuwa ukipita katika mji mkuu wa Monrovia,chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi,mwanamuziki huyo alisema kuwa inasikitisha kuona kwamba hakuna umeme katika barabara ya kilomita 50 kutoka uwanja wa ndege.
Image
Mambo saba ambayo ni marufuku Ethiopia 18 Oktoba 2016 Mshirikishe mwenzako Image copyright REUTERS Image caption Ghasia za hivi karibuni zimejiri kufuatia mauaji ya watu 55 katika tamsaha la kidini la Oromia Serikali ya Ethiopia imetangaza miezi sita ya hali ya tahadhari kufuatia wimbi ambalo halikutarajiwa la maandamano na ghasia. Wanaharakati katika eneo la Oromia wamekuwa wakifanya maandamano tangu November mwaka jana, na waandamanaji kutoka eneo la Amhara wamejiunga kati. Vifo vya watu 55 katika tamasha la kidini la Oromo mnamo Oktoba 2 yalisababisha ghasia kuzuka upya, ikiwemo kulengwa kwa biashara za raia wa mataifa ya nje. Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema watu 500 wamefariki katika maandamano hayo kwa jumla na wiki iliopita waziri mkuu Hailemariam Desalegn amesema huenda idadi hiyo ikawa ya sawa. Hali hiyo ya tahadhari ilitangazwa mapema mwezi huu lakini serikali sasa imeeleza wazi ina maana gani kihalisia: Hizi ndio baadhi ya marufuku: 1.  Mitandao ya kijamii I...

Clinton na Trump: Nani anaongoza?

Image
Wamarekani watapiga kura tarehe 8 Novemba kumchagua rais atakayemrithi Barack Obama wa chama cha Democratic. Hapa tutakupatia tathmini ya udadisi wa kura za maoni nchini humo, hasa kuhusu ushindani kati ya mgombea wa Democratic Hillary Clinton na mwenzake wa Republican Donald Trump. Baada ya mdahalo, huchukua siku kadha kabla ya matokeo yake kudhihirika kwenye kura za maoni. Image caption Utathmini wa kura za maoni kufikia 20 Oktoba, 2016. Kura za maoni zina umuhimu? Ni vigumu kubaini maoni ya watu zaidi ya 300 milioni lakini watafiti wa maoni bado hujaribu. Watu wanaotumiwa huwa ni 1,000 hivi na kwa kuzingatia maadili ya utafiti na sayansi, huwezekana kubashiri matokeo. Majimbo yanayoshindaniwa sana ? Kuna majimbo 13 ambayo yanatarajiwa kushindaniwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Hapa chini ni ramani ya majimbo hayo na uwezekano wa nani atashinda kwa kutumia matokeo ya kura ya maoni ya tovuti ya Real Clear Politics. Ndipo Donald Trump aweze kupata nafasi nzuri, anahitaji kujishind...

Clinton na Trump wataniana kwenye dhifa New York

Image
Image copyright AP Image caption Hafla hiyo huchangisha mamilioni ya dola kusaidia watoto wasio na uwezo na watu maskini Wagombea wakuu wa urais nchini Marekani Hillary Clinton na Donald Trump walirushiana vijembe kwa utani katika dhifa ya jioni iliyoandaliwa kuchangisha pesa za hisani. Walishiriki kwenye dhifa hiyo siku moja baada ya kushambuliana vikali kwenye mdahalo wa mwisho wa runinga. Bi Clinton alicheka sana Bw Trump alipomtania kuhusu hotuba za kulipwa na pia uchunguzi wa FBI kuhusu tuhuma kwamba alitumia barua pepe ya kibinafsi kwa shughuli rasmi. Lakini Bw Trump alizomewa alipofanya mzaha kwamba mpinzani huyo wake huwachukia Wakatoliki. Dhifa hiyo ya Wakfu wa Ukumbusho wa Alfred E Smith mjini New York hufanyika kila baada ya miaka minne na kuwashirikisha wagombea urais. Kuna desturi kwamba wagombea husimama na kutaniana, lakini mwana huu imeandaliwa wakati kumekuwa na uhasama mkubwa sana kwenye kampeni. Trump v Clinton: Nani anaongoza? Trump: Kura zinaibiwa vituoni Marekani ...

Popular This Month

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya