Posts

Showing posts with the label tanzania

Utafiti: Tembo ndio mnyama anayelala kwa muda mfupi zaidi duniani

Image
Wanasayansi waliowafuatilia ndovu wawili nchini Botswana wamebaini kuwa wanyama hao hulala muda mfupi zaidi ya mnyama mwengine yeyote duniani. Ndovu hulala kwa saa mbili pekee hususan nyakati za usiku. Wakiwa katika hifadhi, ndovu hulala kati ya masaa manne hadi sita kwa siku. Mbwa achaguliwa tena kuwa meya Minnesota, Marekani Wanyama waliowahi kushinda nyadhifa uchaguzini Ndovu hao wote wakiwa viongozi wa familia zao mara nyengine husalia macho kwa siku kadhaa na huonekana wakifunga macho ama kuota mara moja kila siku tatu ama hata nne. Haijulikani kwa nini wanyama hao walio na uwezo mkubwa wa kukumbuka vitu wanaweza kuishi kwa kulala kwa muda mfupi licha ya usingizi kuwa na muhimu mkubwa katika ubongo .

FIFA: Argentina bado wababe, Tanzania washuka

Image
Image copyright AFP Image caption Argentina wameendelea kuongoza orodha hiyo ya ubora Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka duniani, ambapo vinara wamesalia kuwa Argentina. Wanafuatwa kwa karibu na mabingwa wa dunia Ujerumani, kisha Brazil wanashika nafasi ya tatu. Ubelgiji imeshuka nafasi mbili hadi nambari nne. Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi. Tanzania sasa inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka nafasi 12. Uganda wamo nambari 72 baada ya kushuka nafasi saba, Kenya wamepanda nafasi sita hadi nambari 85 nao Rwanda wamesalia nambari 107. Ethiopia wamo nafasi ya 126, Malawi 100 na Burundi 138. Nchi ya juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32. Orodha nyingine ya Ubora wa viwango itatolewa Novemba 24. Mataifa 10 bora duniani 1.Argentina 2.Ujerumani 3.Brazil 4.Ubelg...

Sababu ya Mfalme wa Morocco kuzuru Tanzania

Kwa mara ya kwanza, Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, Jumapili hii anaitembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi baada ya kuzuru Rwanda. Miongoni mwa ajenda kuu za ziara yake ni kuishawishi Tanzania kuiunga mkono Morocco kurejeshwa katika Umoja wa nchi za Afrika. Aidha, atatia saini mikataba ya kibiashara na kidiplomasia kati ya Tanzania na Morocco. Mfalme Mohammed VI pia atazuru pia Ethiopia. Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Arnold Kayanda amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga na kuandaa taarifa hii.

Sababu ya Mfalme wa Morocco kuzuru Tanzania

Kwa mara ya kwanza, Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, Jumapili hii anaitembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi baada ya kuzuru Rwanda. Miongoni mwa ajenda kuu za ziara yake ni kuishawishi Tanzania kuiunga mkono Morocco kurejeshwa katika Umoja wa nchi za Afrika. Aidha, atatia saini mikataba ya kibiashara na kidiplomasia kati ya Tanzania na Morocco. Mfalme Mohammed VI pia atazuru pia Ethiopia. Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Arnold Kayanda amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga na kuandaa taarifa hii.

Bendera: Tanzania yaishutumu Korea Kaskazini kwakutumia bendera yake kinyume na sheria

Image
Image copyright AFP Image caption Tanzania imefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria. Taifa la Tanzania limefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria. Waziri wa maswala ya kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga aliambia BBC kwamba meli hizo zilionekana hivi karibuni katika bahari hindi eneo ambalo halipo mbali na Tanzania. Hatahivyo hakutoa idadi kamili ya meli hizo. ''Meli za Korea Kaskazini zilipigwa marufuku na Umoja wa Mataifa na hazikuruhusiwa kusafiri ama hata kutia nanga'',alisema Mahiga. ''Kwa hivyo meli hizi zimekuwa zikijaribu kutafuta njia kukiuka vikwazo hivyo ili kuweza kuendelea na biashara zao,na mbinu moja ni kupeperusha bendera za mataifa tofauti''. Waziri huyo amesema kuwa malalamishi yametumwa katika serikali ya Korea Kaskazini wakilaumu biashara hiyo ya ujanja. ''Shirika la kimataifa la ma...

Zitto awasilisha muswada mafuta, gesi ya Zanzibar

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amewasilisha rasmi muswada binafsi wa Sheria ya Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu mafuta na gesi ya Zanzibar. Zitto amesema amefanya hivyo katika kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia wa  ACT Wazalendo uliofanyika Oktoba 2016, baada ya mjadala wa mada kuhusu Zanzibar na Katiba ya Muungano. Zitto alisema hoja hiyo inakuwa muhimu kwa sasa kwa sababu ya kunusuru uvunjwaji wa Katiba ulio wazi. “Kusubiri Katiba Mpya hakuhalalishi iliyopo kuvunjwa. Kwa kuwa mabadiliko ya Katiba Mpya yamekwama bila ya kauli ya Serikali kujua lini mchakato utaendelea, hii hoja yetu ni ya lazima kwa sasa katika kuhalalisha hatua ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kutunga sheria inayohusiana na mafuta na gesi asilia,” alisema Zitto.

Harufu ya feri yakimbiza wateja

Image
Dar es Salaam.  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema amesema harufu mbaya inayotoka kwenye soko la samaki la feri inasababisha baadhi ya wateja wasifike sokoni hapo kununua samaki. Akikabidhi bodi mpya ya soko hilo, Mjema amesema wateja wasipofika kununua samaki mapato ya soko yanapungua na kusababisha soko liendelee kuchakaa. Ameipa bodi mpya ya soko hilo miezi mitano kumaliza tatizo la harufu hiyo na kuongeza mapato vinginevyo ataivunja.Mkuu wa wilaya alielezwa na Meneja wa Soko, Nico Eliakimu kuwa wanakusanya ushuru wa Sh 105 milioni kwa mwezi

Panya Road wa Mbagala watiwa mbaroni

Image
Dar es Salaam.  Jeshi la polisi mkoa wa Temeke limewakamata watu zaidi ya 15 wanaodaiwa kuwa ni Panya Road waliovamia na kuwapora  watu waliokuwa wakitoka kwenye tamasha la kuinua vipaji lililoandaliwa na redio ya  Clouds. Wahalifu hao wanadaiwa kufanya uhalifu rmaeneo ya Sabasaba, Temeke, huku wakiwa na silaha za kijadi ikiwamo mapanga maeneo ya Sabasaba. Kamanda wa polisi mkoa huo,Gilles Muroto alisema Oktoba 15 saa 11 jioni  liliandaliwa  tamasha la kuinua vipaji na Clous FM ambapo vijana hao walishiriki na baadaye kufanya uhalifu huo. Alisema baada ya tamasha hilo kwisha watuhumiwa hao wanaodaiwa kuwa zaidi ya 50 waliingia mtaani huku na kuelekea eneo la sabasaba wakiwa na mapanga,visu,bisibisi kwa ajili ya kufanyia uhalifu. Muroto alisema wakati wakielekea eneo hilo ndipo wananchi waliwadhibiti na kuwakamata vijana sita kati ya hao mmoja alifariki wakati akipelekwa hospitali,wawili wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya temeke na watatu walitoa ushirikiano ...

Upepo waezua shule, watoto sita wajeruhiwa

Image
Picha na Phinias Bashaya,  Mwananchi Missenyi.  Upepo mkali umeezua vyumba sita vya madarasa karika Shule ya Msingi Byamutemba wilayani hapa mkoani Kagera na kujeruhi wanafunzi sita. Kutokana na tukio hilo lililoathiri pia nyumba za wakazi wa eneo hilo ambazo idadi yake haijafahamika, Serikali imeifunga kwa muda usiojulikana shule hiyo, ikisubiri kuijenga baada ya taratibu kukamilika. Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Limbe Mourice amesema majeruhi hao wamelazwa katika Kituo cha Afya Bunazi. Kwa siku za karibuni Mkoa wa Kagera umekumbwa na mabalaa likiwamo tetemeko la ardhi liliua watu 17 na kusababisha nyumba zaidi ya 3,000 kuanguka na hadi sasa nyingi hazijajengwa.

JPM atengua uteuzi wa mkurugenzi wa Mkinga

Image
Dar es Salaam.  Siku moja baada ya kushtakiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga, Emmanuel Mkumbo, Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi huyo kuanzia leo Jumanne. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa uteuzi wa takayejaza nafasi ya Mkumbo utafanywa baadaye. Mkumbo alishtakiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwa makosa mawili ambayo ni la kudaiwa kutishia kuua na makosa ya usalama barabarani.

Wanawake wawili wamshtumu Donald Trump kuwapapasa kimapenzi

Image
na RFI Donald Trump, akiwa na bango mkononi lililoandikwa "wanawake pamoja na Trump", katika mkutano wa hadhara mjini Lakeland, Oktoba 12, 2016. REUTERS Gazeti la New York Times limechapishwa Alhamisi hii asubuhi ushahidi wa wanawake wawili ambao wanasema kuwa walishambuliwa kingono na Donald Trump. Mgombea urais wa chama cha Republican tayari ameumbuka na video ya mwaka 2005 ambapo anazungumzia mambo ya uasherati. Watu wengi nchini Marekani wanajiuliza kwa nini Donald Trump hakusikia ushauri mwema kutoka kwa wajumbe wa chama cha Republican kwa ajili yake, wale waliomshauri kufunga ukurasa wa kauli zake za uasharati na hivyo kuomba tu radhi kwa yale yaliyotokea? Mgombea huyo aliamua kulipiza kisasi, na kutoa wito katika mjadala wa mwisho kwa makahaba wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton katika mwaka mwaka 1990. Matokeo ya kauli ya Bw Trump yameanza kujitokea. Wanawake leo wanamshtumu mgombea urais wa chama cha Republican aliwapapasa kimapenzi pila idhni yao. Katika gaze...

Wasiwasi waendelea Duniani kuhusu simu hatari ya Galaxy note 7

Image
Samsung kuwatumia wateja wake walioko Marekani makasha yanayoweza kustahimili moto, kuweka Note 7 wanazorejesha Kampuni ya vifaa vya eletroniki ya Samsung imetangaza kuwatumia wateja wake walioko Marekani makasha yanayoweza kustahimili moto, kama tahadhari dhidi ya uwezekano wa kutokea moto au kulipuka kwa simu zake aiana ya Galaxy Note 7 walizorejesha kwa wauzaji simu hizo nchini humo. Makasha hayo hasa yanatolewa kwa wateja walionunua simu hizo katika tovuti yake ya Samsung.com. Walio na simu hiyo aina ya Galazy Note 7 pia wameshauriwa kutembelea tovuti ya Samsung kufahamu maelekezo ya kuzirejesha. Kampuni hiyo ya Samsung imetangaza kusitisha utengenezaji wa simu hiyo ya Galazy note 7 miezi miwili baada ya kuizindua upya, baada ya kurekebishwa mara ya pili, kufuatia ripoti kadhaa za simu hiyo kushika moto.Samsung sasa italazimika kupokea zaidi ya Galazy Note 7 million 1.5 ilizokuwa tayari imeuza au kutoa kama simu mbadala. Nyingi ya simu hizo ziliuzwa Marekani na Korea Kusini. Hata i...

MWALIMU ASAKWA NA POLISI KILIMANJARO KWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

Image
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa By Fina Lyimo na Bahati Chume, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz Hai . Polisi mkoani Kilimanjaro  inamsaka mwalimu wa Shule ya Sekondari Lemira wilayani hapa anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne na kukimbilia kusikojulikana. Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa mzazi wa mwanafuzi huyo na mkuu wa shule wanashikiliwa ili kusaidia kupatikana kwa mawlimu huyo. Amesema mzazi aligundua kuwa mwanaye ana ujauzito wa miezi mitano na alipomuuliza alimwambia mhusika ni mwalimu wake. “Mzazi wa mtoto alimfuata mwalimu huyo aliyekubali kuwa ujauzito ni wake na kwamba atamuoa. Alimtaka aweke kwenye maandishi kuwa ujauzito ni wake na atamuoa,” alisema Mutafungwa. Amesema mwalimu huyo alikubali na kuandika kuwa atamuoa mwanafuzi atakapojifungua na kwamba, mkuu wa wilaya alipopata habari hizo alizifuatilia ili kujua sababu. Alisema alipoitwa kwa mkuu wa wilaya, mwalimu huyo a...

Ngassa afunga Goli lake la kwanza akicheza Fanja FC ya Oman

Image
MICHEZO Winga wa kimataifa wa  Tanzania anayecheza soka katika klabu ya  Fanja FC ya  Oman   Mrisho Ngassa   amefanikiwa kuanza maisha yake mapya ya soka katika klabu hiyo kwa kufunga goli akicheza mchezo wake wa kwanza toka ajiunge na klabu hiyo. Ngassa  ambaye amejiunga na  Fanja FC akiungana na aliyekuwa mshambuliaji wa Simba   Danny Lyanga  amefunga goli katika mchezo dhidi ya  Al-Nahda , mchezo ambao umemalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2.

TANZANIA MIAKA SABA BILA NYERERE NININI TULICHO MISS?

Image
Wakati  Tanzania leo ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 17 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema Taifa limepoteza mwelekeo  kwani halina tena uadilifu aliotujengea Mwalimu Nyerere. Mwinyi aliyerithi mikoba ya urais kutoka kwa Mwalimu Nyerere mwaka 1985, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mdahalo wa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kuzindua kitabu cha 'Selective works of Mwalimu Nyerere', kilichotafsiriwa na wasomi kutoka China. Mdahalo huo uliandaliwa na Taasisi ya Uongozi ikishirikiana na Ubalozi wa China na Asasi ya Urafiki kati ya Tanzania na China. Mwalimu Nyerere aliyeitawala Tanzania kwa takribani miaka 24, alifariki dunia Oktoba 14, 1999 kwenye Hospitali ya St Thomas jijini London nchini Uingereza ambako alikuwa akitibiwa maradhi ya saratani ya damu. Aliiongoza Tanzania kwa uadilifu mkubwa akisimamia misingi ya haki, umoja, mshikamano, kupiga vita rushwa, kusisitiza kujite...

Popular This Month

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya