TAFITI: Wanaosoma habari mitandaoni hupoteza kumbukumbu haraka kuliko magazetini | admin

Share


Kama wewe ni mfuatiliaji na msomaji wa habari mitandaoni basi bila shaka huenda ulishawahi kukumbana na hali ya kusoma habari ambayo baada ya kumaliza ukaanza kukumbuka kama ulishawahi kusoma habari hiyo sehemu fulani lakini umesahau, basi utakuwa upo sahihi kabisa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na muandishi wa habari mkongwe wa Gazeti la Financial Times,  Michael Skapinker amebaini kuwa wasomaji wa habari mitandaoni wengi wao hupoteza kumbukumbu ya kuhifadhi habari walizosoma kwa muda mfupi sana ukilinganisha na wale wanaosoma habari kupitia Magazeti.

Mwandishi huyo amesema asilimia kubwa ya wasomaji wa habari mitandaoni hufikiria zaidi kutoa maoni na kushare habari walizozipenda na sio kutilia maanani kwenye usomaji wa habari.

Utafiti huo uliofanyika kwenye nchi 60 tu umeonesha kuwa wasomaji wengi wa habari mitandaoni wanasoma habari nyingi kwa muda mfupi huku wakifanya shughuli nyingine kitu ambacho kinawafanya wakose umakini wa kuzingatia kile wanachokisoma tofauti kabisa na wale wanaosoma habari kwenye magazeti ambao hupaswa kupumzika kabisa ili kuweza kusoma gazeti.

Kwenye nchi 60 alizofanya utafiti huo, Michael Skapinker amesema kuwa asilimia 85 ya vijana chini ya miaka 40 ndiyo wanaopendelea zaidi kusoma habari za mitandaoni huku 15% wakisoma habari kupitia Majarida na Magazeti.

Hata hivyo utafiti huo umeonesha ingawaje vijana wengi wanasoma habari mitandaoni ila ni wepesi sana kusahau habari walizoma yaani kupoteza kumbukumbu kwa muda mfupi ukilinganisha na wale wanaosoma habari kwenye Magazeti.

Utafiti huo pia umeonesha kuwa ingawaje kuna ongezeko kubwa la wasomaji wengi wa habari mitandaoni lakini bado kuna kundi la wasomaji hawaamini habari hizo mpaka wazikute kwenye magazeti.

Bwana Skapinker amesema ingawaje wasomaji wa mtandaoni hupoteza kumbukumbu haraka lakini bado watu wengi huvutiwa na habari za mitandaoni kutokana na uharaka wa kuzipata, kuokoa muda, kupunguza gharama na urahisi wa kutoa maoni ya walichokisoma.

READ MORE

Share



from AutoMedia Tanzania
via Read More

Comments

Popular This Week

TFF YAIKOMALIA YANGA, YAITAKA IFANYE UCHAGUZI KUZIBA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI. | Darmpya

Halotel wazindua huduma ya mpya ya Chips bando ndani ya Sabasaba | Andrew Chale

WOLPER AKINUKISHA TENA. | Darmpya

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

Popular This Month

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Halotel wazindua huduma ya mpya ya Chips bando ndani ya Sabasaba | Andrew Chale

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 11, 2017 | Pamoja Blog

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

TFF YAIKOMALIA YANGA, YAITAKA IFANYE UCHAGUZI KUZIBA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI. | Darmpya

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya