TFF YAIKOMALIA YANGA, YAITAKA IFANYE UCHAGUZI KUZIBA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI. | Darmpya
Shirikisho la Kabumbu nchini Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kufanya uchaguzi ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na viongozi wake waliojiuzuru, akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.
Hayo yamebainishwa mapema siku ya leo kupitia barua ya Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Herman Julius kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho hilo, Revocatus Kuuli, iliyoitaka klabu ya yanga kufanya uchaguzi huo kama sheria na kanuni za mpira nchini zinavyotaka.
Katika barua hiyo ya Herman Julius, klabu zingine zilizotakiwa kufanya uchaguzi ili kujaza nafasi za uongozi ni AFC ya Arusha na Coastal Union ya Tanga.
Klabu ya Yanga imekuwa ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga, kwa takribani mwaka mmoja sasa kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti Yusuf Manji mwezi Mei mwaka jana.
from Dar Mpya Online TV
Comments