Posts

Showing posts with the label Dar Mpya Online TV

CUF UPANDE WA MAALIM SEIF WAMUANGUKIA JAJI MKUU | Darmpya

Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa katibu mkuu Maalim Seif Sharif Hamad kimemuomba Jaji Mkuu na Jaji kiongozi kusaidia kusomwa hukumu katika shauri linalohusu uhalali wa uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba. Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam  na Mnadhimu wa Kambi ya CUF Bungeni ambaye pia ni mbunge wa Malindi Ally Saleh wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema shauri hilo lililopo mbele ya Jaji Dr.Benhajj Massoud tayari limeshasikilizwa kwa pande zote mbili na lipo katika hatua ya kutolewa hukumu. Mnadhimu huyo amesema kuwa kucheleweshwa kutolewa kwa hukumu hiyo kumeathiri… Source from Dar Mpya Online TV

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

Na Amiri kilagalila Takribani ya vijiji 20 vilivyopo kata 6 wilayani ludewa mkoani Njombe vinatarajia kunufaika na mradi wa umeme wa megawati 1.6 uliopo katika kijiji cha Lugalawa wilayani humo. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mara baada ya kutembelewa na barozi wa nchi ya Ujerumani nchini Tanzania DETLEF WACHTER,Mkuu wa mkoa wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA amesema kuwa mradi huo wa kufua umeme kwa kutumia maji unatarajia kukamilika mwezi aprili mwaka huu. “ni kwamba tuna mradi wa kufua umeme kwa kutumia maji katika kijiji cha Lugalawa wilaya ya Ludewa… Source from Dar Mpya Online TV

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUMALIZA TATIZO LA VYUMBA VYA MADARASA | Darmpya

Na Allawi Kaboyo. kufatia kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa na kupelekea uwepo wa mrundikano wa wanafunzi katika shule za sekondari Tunamkumbuka na Butulage zilizopo halmashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera, wananchi katika maeneo hayo waliamua kuanzisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa kila shule ambapo serikali imewaunga mkono kwa kuwapelekea kila shule shilingi milioni 25 ili kumalizia ujenzi huo. Akiwaelezea wananchi upatikanaji wa fedha hizo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi ulipofikia Februari 25 mwaka huu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa kata… Source from Dar Mpya Online TV

BILIONI 1.2 ZA BENK YA NMB KUTUMIKA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU KANDA YA ZIWA VICTORIA | Darmpya

Na mwandishi wetu Benki ya NMB kanda ya ziwa Victoria inatarajia kutumia zaidi ya Sh1.2 bilioni kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika sekta ya elimu na afya kwenye mikoa iliyoko ndani ya kanda hiyo Kaimu meneja wa NMB wa kanda ya ziwa Abrahim Agustino alisema fedha hizo zinatumika kuweka samani katika shule za msingi na sekondari na kuboresha miundombinu katika vituo vya afya na Hospitali pale wananchi na viongozi wanapopeleka ombi la kusaidiwa nguvu zao Agustino alisema hayo jana wakati akikabidhi meza 62 na viti 62 vyenye thamani ya Sh… Source from Dar Mpya Online TV

SERIKALI YAUNGANA NA WANANCHI UJENZI WA MADARASA | Darmpya

from Dar Mpya Online TV

MAHAKAMA YASOGEZA MBELE KESI YA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE | Darmpya

Na Amiri kilagalila Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe leo imewapandisha kizimbani kwa mara ya pili watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto watatu wa familia moja wa kijiji cha Ikando kata ya kichiwa wilayani Njombe. Watuhumiwa hao ni JOEL JOSEPH NZIKU,NASSON ALFREDO KADUMA na ALPHONCE EDWARD DANDA ambao Wanakabiliwa na mashtaka ya kuwaua watoto hao kijijini humo. Watoto hao ni Godliver Nziku, Gasper Nziku na Giriad Nziku ambao ni watoto wa familia moja huku ikielezwa kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa la kuwaua januari 20 mwaka huu. hakimu mkazi mkoa… Source from Dar Mpya Online TV

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya

Na Amiri kilagalila Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Njombe limewataka Mafundi wanaojihusisha na shughuli za nishati ya umeme mkoani humo kupata leseni kutoka mamlaka ya uthibiti wa nishati na maji EWURA ili kupambana na mafundi wasiokuwa na weledi na kazi zao wala kutambulika kisheria huku wakisababisha matatizo kwa wateja. Wito huo umetolewa na mhandisi wa mpango na kaimu meneja wa Tanesco mkoa wa njombe, YUSUPH SALIM wakati akizungumza na mafundi umeme pamoja na wahandisi katika mkutano wa pamoja ulioandaliwa na umoja wa makandarasi (UMAU) katika ukumbi wa Miriam… Source from Dar Mpya Online TV

MBALONI KWA KUMCHOMA MOTO MTOTO SABABU YA UDOKOZI | Darmpya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Eliza Denis (23) mkazi wa Makulu mkoani hapo kwa tuhuma za kumpiga sehemu mbalimbali za mwili na kumchoma moto mikononi mtoto wake wa kambo, Jackson Denis (5) kwa madai ya kudokoa chakula. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku jeshi la polisi likimshikilia mama huyo. “Huko maeneo ya Dodoma Makulu amekamatwa mama mmoja ajulikanae kwa jina la Eliza Denis ambaye ni mkulima na mkazi wa Dodoma Makuli kwa makosa ya kumpiga sehemu mbalimbali za mwili na… Source from Dar Mpya Online TV

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

Na Shabani Rapwi Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Saimon Msuva anaekipiga katika klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco usiku wa jana Jumamosi ametupia magoli mawili na kuifanya timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Ittihad Tanger katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Morocco (Botola Pro League). Msuva alifunga goli la kwanza dakika ya 2′ na dakika ya 30′. Ushindi huo wa magoli 2-0 unaifanya Difaa El Jadida kufikisha alama 24 wakiwa nafasi ya 9 huku Ittihad Tanger wakibaki nafasi ya 3 wakiwa na alama 27… Source from Dar Mpya Online TV

AZAM FC YAWATANGAZA MAKOCHA WAWILI, BAADA YA KUACHANA NA HANS | Darmpya

Na Shabani Rapwi. Uongozi wa klabu ya Azam FC jana Jumamosi, February 23, 2019 ulimetangaza rasmi kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Hans Van Der Pluijm baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili. Azam FC imefikia makubaliano ya kuachana na Hans pamoja na Msaidizi wake, Juma Mwambusi kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya hivi karibuni kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Katika mechi 5 za mwisho chini ya kocha Hans wamefungwa mechi 2 (Tanzania Prison 1-0 na Simba 3-1 ) na kutoa sare mechi 3… Source from Dar Mpya Online TV

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick L. Mpogolo amewataka viongozi wa Mkoa wa Dodoma na wana CCM kwa ujumla kushiriki katika vikao vya mashina na kuimarisha mashina wanayotokana nao ili kukiongezea mtaji Chama cha Mapinduzi. Ndg Mpogolo ameyasema hayo leo Wilaya ya Dodoma Mjini wakati wa maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa CCM kwa kuagiza Viongozi wote bila kujali nafasi zao kushiriki katika vikao vya mashina na kuwatambua mabalozi wao na kuwapa ushirikiano unaostahili kwa ustawi wa Chama. Akiwa katika ziara katika kiwanda cha Mvinyo cha CETAWICO ,Ndg Mpogolo… Source from Dar Mpya Online TV

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Waziri wa Nishati Mhe. Medard Kalemani kwenye ziara ya kikazi mkoani Mwanza iliyoanza hii leo akiwa wilayani Nyamagana amewasha mradi wa umeme Vijijini REA mtaa wa Nyakagwe katika Kata ya Buhongwa. Mhe. Kalemani amesema, serikali ya Mhe. John Pombe Magufuli imeongezewa KM 20 za ziada kutoka KM 25 zilizokuwepo awali Nyamagana katika mpango wa mradi wa umeme Vijinini REA na kufikia KM 45 ikiwa ni ombi maalum la Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ili kutatua changamoto ya umeme kwa wakazi walioko maeneo ya pembezoni. Akiongea na wananchi… Source from Dar Mpya Online TV

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWASHUKIA WAAJIRI WANAOKWEPA KODI KWA KUDANGANYA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI | Darmpya

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewashukia waajiri wote wanaotoa taarifa ambazo si sahihi za mishahara ya wafanyakazi kwa lengo la kukwepa kodi na pia kuchangia mchango mdogo katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii tofauti na mshahara wake. Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Anthony Mavunde wakati akiongea na waandishi wa habari katika Jiji la Mbeya na kubainisha kwamba Ofisi ya Kamishna wa Kazi inaendelea na ukaguzi wa kawaida ili kuwabaini waajiri hao na kuwachukulia hatua za… Source from Dar Mpya Online TV

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Zaidi ya tani 68 za Korosho zilizokuwa zimepimwa na wakulima katika vyama vya Msingi Chemana na China kata ya Chitekete Halmashauri ya wilaya Newala Mkoani Mtwara, zimerejeshwa kwa wakulima baada ya kukataliwa na Meneja wa maghala kuingizwa kwenye maghala makuu ya TANECU- Newala kwa kinachodaiwa kukosa ubora. Mwenyekiti wa chama cha Msingi Chemana Abilahi Ibadi, amesema Korosho zilizorejeshwa kwa wakulima ni tani 15.6 Kwa upande wake Mwenyekiti msaidizi wa chama cha Msingi China Juma Samli, amesema Korosho zilizorejeshwa kwa wakulima walio chini yake ni Tani 53… Source from Dar Mpya Online TV

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

Na Shabani Rapwi. Usiku wa kuamkia leo Jumamosi, February 23, 2019, mabondia wawili wa Tanzania, Hussein Itamba, Ibrahimu Tamba walikuwa ulingoni katika mji wa Budepest, Hungary na wote wamepoteza mpambano yao kwa points. Pambano la kwanza lilikuwa la raundi nane la uzito wa Middle Weight 77’5kgs kati ya Hussein Itamba dhidi ya mjerumani Mates Kids, na mtazamani Itamba alipoteza kwa pambano ilo kwa points zaidi ya mjerumani huyo. Na pambano la pili lilimkutanisha bondia mtanzania Ibrahim Tamba na bondia Sherfat Suf kutoka Hurungay katika pambano la raundi nane uzito wa… Source from Dar Mpya Online TV

SERIKALI KURASIMISHA UJUZI KWA MAFUNDI ZAIDI YA 10,000 NCHINI KUTUMIA PROGRAMU YA MFUMO WA UTAMBUZI NA URASIMISHAJI UJUZI(RPL) | Darmpya

Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira katika utekelezaji wa programu ya RPL imedhamiria,katika awamu ya kwanza, kuwafikia na kurasimisha ujuzi kwa takribani watanzania 10,000 kwa Mwaka 2019/2020. Hayo yamesemwa leo katika ukumbi wa Royal Tughimbe jijini Mbeya na Naibu Wziri Ofisi ya Waziri mkuu kazi,vijana na ajira mh Anthony Mavunde, wakati akifungua kongamano la mafundi wa Mkoani Mbeya,ambapo alibainisha kwamba serikali inatekekeleza programu ya kurasimisha ujuzi kwa watu wenye ujuzi lakini ambao hawajapitia katika mfumo rasmi wa mafunzo ya ufundi kwa kuwapatia vyeti vya Ufundi pasipo wao kusoma chuo… Source from Dar Mpya Online TV

EWURA KUANZISHA VITUO VYA MAFUTA VYA KUHAMA HAMA | Darmpya

Na Amiri kilagalila Ili kurahisisha upatikanaji wa nishati ya mafuta mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA imesema kuwa inataraji kuanzisha huduma ya sheli zinazotembea Mobile pump station kwa kutumia magari maalumu yalitengenezwa kwa kazi hiyo zikiwemo pikipiki za miguu mitatu zinazoendelea kuundwa kupitia chuo kikuu cha dar es salaam udsm. Mkurugenzi wa mawasiliano na mahusiano mamlaka ya udhibiti ya nishati na maji Titus kaguo ameyasema hayo wakati akijibu maswali ya baadhi ya wadau wa nishati na maji walioshiriki katika semina elekezi juu ya ufanyaji kazi wa mamlaka hiyo… Source from Dar Mpya Online TV

DC MJEMA AWATAKA WATENDAJI KWENDA NA KASI YA JPM | Darmpya

Na Heri Shaban MKUU wa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amewataka watendaji wa Manispaa ya Ilala kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Ilala. Mjema aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam katika kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekekezaji wa Ilani cha chama cha Mapinduzi CCM kuanzia Januari 2018 hadi Disemba 2018. “Dhamana tulizopewa siyo kwa ajili yetu bali ni kwa ajili ya wananchi. Rais wetu ana matumaini makubwa kutoka kwetu kwamba tutawajibika katika majukumu yetu ili kuleta maendeleleo na kuifikia ndoto yake ya kuinua… Source from Dar Mpya Online TV

ARSENAL YATINGA HATUA YA 16 BORA, EUROPA LEAGUE | Darmpya

Na Shabani Rapwi. Usiku wa jana, Arsenal wametinga hatua ya 16 bora ya Europa League baada ya kupata ushindi wa magoli 3-0 na kufanya kuwa jumla ya magoli 3-1 dhidi ya Bate Borisov baada ya mechi ya kwanza kufungwa goli 1-0, Goli la kwanza la Arsenal likipatikana dakika ya 4 baada ya nyota wa Bate, Voikov kujifunga, dakika ya 39 Shdaran Mustafi alipachika goli la pili na dakika ya 60, Sokratic Papastar alipachika goli la tatu na la ushindi. Arsenal inaungana na timu za, Sevilla, Napoli, Valencia, Villarreal, Dinamo Zagreb,… Source from Dar Mpya Online TV

WANA CCM MAWAKALA WA RUSHWA MKOA WA IRINGA WAONYWA | Darmpya

Na Francis Godwin, Iringa CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimewaonya watendaji wa chama hicho pamoja na wale wa kuchaguliwa kufanya kazi walizoomba badala ya kuanzisha vurugu za kujipanga kwa uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020 na baadhi yao kuwa mawakala wa usambazaji rushwa za wagombea. Kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao kwa sasa wanashindwa kuwajibika kwa shughuli za chama na badala yake wamekuwa wakihangaika na kujiandaa kwa ajili ya kugombea nafasi za juu kama udiwani na ubunge huku wakitambua muda wa kufanya hivyo bado haujafika . Akizungumza na viongozi… Source from Dar Mpya Online TV

Popular This Month

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya