Halotel wazindua huduma ya mpya ya Chips bando ndani ya Sabasaba | Andrew Chale
Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel leo Julai 7, 2017, imezindua rasmi huduma mpya ya CHIPSI BANDO yenye kauli mbiu ‘Serereka na Chipsi bando, tumia upendavyo” ambapo wateja wote wa Halotel watapata fursa ya kujiunga kwa bei rahisi ya Tsh. 100 pekee.
Wakieleza namna ya huduma hiyo mpya ya Chipsi bando, ndani ya maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara kwenye mabanda ya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam, ambapo wamesema kuwa, lengo ni kumwezesha kila mtanzania kufurahia huduma bora na kwa bei nafuu kabisa katika thamani ya pesa yake kwa kupata muda wa maongezi na data za intaneti.
Huduma hiyo, mteja anaweza kujiunga kwa lisaa limoja kwa Tsh. 100 na kuweza kupata: Dakika za kwenda mitandao ya Halotel kwenda Halotel sekunde 200.
Pia kwa Tsh 100, kwa lisaa limoja mteja anaweza kupata dakika za kwenda mitandao mingine, sekunde 100, huku pia kwa Tsh. 100 hiyo hiyo, mteja kwa lisaa limoja, anaweza kupata huduma ya data ambayo ni MB 25.
Pia mteja kwa thamani ya Tsh. 100, anaweza kupata Halotel kwenda Halotel kuongea bila kikomo, kuanzia saa sita usiku mpaka saa 12 asubuhi.
“Mteja anaweza kujiunga kwa kupiga *148*66#. Ambapo atapata orodha ya huduma atakayopenda kati ya hizo. Ambapo anaweza kuchagua huduma namba mbili katika orodh na atapata Chipsi bando na kuweza kujiunga. Hii ni kwa wateja wote wa mtandap wa Halotel popote pale walipo” walieleza Halotel.
Halotel pia inatoa huduma mbalimbali kwenye maonyesho hayo ikiwemo simu za mkononi na nyingine nyingi.
from AutoMedia Tanzania
via Read More
Comments