Obama asikitishwa na malalamiko ya Trump

Rais Barack Obama wa MarekaniImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionRais Barack Obama

Rais Barack Obama wa Marekani ameyaelezea malalamiko yaliyotolewa na mgombea kupitia chama cha Republican, Donald Trump, kwamba kuna udanganyifu unafanyika katika uchaguzi wa Rais nchini humo, kuwa ni ya hatari na kuharibu demokrasia.

Amemlaumu mgombea huyo wa Republican kutilia shaka uhalali wa uchaguzi huo, bila ya kuwa na ushahidi kamili wa kuwepo kwa hila kwenye uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

Wakati wa mdahalo wao wa tatu na wa mwisho uliofanyika jana katika yake na mpinzani wake Hillary Clinton, Bwana Trump alikataa moja kwa moja kusema kwamba atakubali matokeo iwapo atashindwa.

Hata hivyo chama chake cha Republican kimekuwa kikijaribu kusafisha kauli yake hiyo.

Timu ya Kampeni ya uchaguzi ya Bwana Trump inamlaumu Hillary Clinton mgombea kupitia chama cha Democrats kwa kupanga jaribio la kutaka kumchafua mgombea huyo wa Republican baada ya mwanamke wa 10 kujitokeza akiilaumu tabia yake ya kudhalilisha wanawake kijinsia.

Mwana mama huyo Karena Virginia anamtuhumu Bwana Trump kwa kile alichosema alimpapasa kifuani, wakati wa mashindano ya mchezo wa tenisi mwaka 1998.

Comments

Popular This Week

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

Popular This Month

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya