Posts

Showing posts with the label kimataifa

Samatta kaifungia KRC Genk goli mbili vs Club Brugge katika ushindi wa 2-1 (+Video)

Image
Usiku wa March 4 2017  nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta aliingia katika uwanja wao wa nyumbani wa Luminus Arena kuitumikia club yake ya KRC Genk katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya vinara wa Ligi hiyo Club Brugge . Katika mchezo huo KRC Genk ambao walikuwa nyumbani walifanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1, magoli ya KRC Genk yakifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 5 na 42, katika magoli yote aliyofunga Samatta alipewa pasi na Malinovsky na Alejandro Pozuelo , huku goli la Brugge likifungwa na Izquierdo dakika ya 43. Matokeo hayo yanaifanya KRC Genk kuendelea kuwa nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji wakiwa na point 45, wakati Club Brugge wao wakiendelea kuongoza Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 kwa kuwa na jumla ya point 58 sawa na Anderlecht waliyo nafasi ya pili. source: millardayo.com

Utafiti: Tembo ndio mnyama anayelala kwa muda mfupi zaidi duniani

Image
Wanasayansi waliowafuatilia ndovu wawili nchini Botswana wamebaini kuwa wanyama hao hulala muda mfupi zaidi ya mnyama mwengine yeyote duniani. Ndovu hulala kwa saa mbili pekee hususan nyakati za usiku. Wakiwa katika hifadhi, ndovu hulala kati ya masaa manne hadi sita kwa siku. Mbwa achaguliwa tena kuwa meya Minnesota, Marekani Wanyama waliowahi kushinda nyadhifa uchaguzini Ndovu hao wote wakiwa viongozi wa familia zao mara nyengine husalia macho kwa siku kadhaa na huonekana wakifunga macho ama kuota mara moja kila siku tatu ama hata nne. Haijulikani kwa nini wanyama hao walio na uwezo mkubwa wa kukumbuka vitu wanaweza kuishi kwa kulala kwa muda mfupi licha ya usingizi kuwa na muhimu mkubwa katika ubongo .

Wanandoa 160 watalakiana China ili kufaidika na fidia

Image
Zaidi ya wanandoa 160 wanaoishi katika kijiji kimoja kusini mwa China wameama kutalakiana kwa lengo kupata kiwango kikubwa cha fidia itakayolipwa baada ya nyumba zao kuvunjwa kwa nguvu. Kijiji hicho cha Jiangbei mashariki mwa China kinavunjwa ili kutoa nafasi ya ujenzi. Wanandoa wanaoishi katika eneo hilo waligundua kwamba watafaidika na ujenzi wa nyumba mbili na takriban dola elfu 19 iwapo wataachana na kudai fidia hiyo wakiwa mbali mbali. Baadhi ya wanandoa hao wana zaidi ya miaka 80, na wengi walisema walipanga kuendelea kuishi.

Asema alilazimishwa kukiri kumuua Kim Jong nam na Malaysia

Image
Mtu mmoja anayeshukiwa kuhusika na mauji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amesema kuwa yeye ni mhanga wa hujuma za utawala wa Malaysia dhidi ya Korea Kaskazini. Akizungumza mjini Beijing baada ya kuwasili kutoka Malaysia, Ri Jong Chol, amelaumu polisi wa Malaysia, kwa kutishia familia yake, iwapo hatakiri kuhusika kwake na mauaji ya Kim Jong Nam. Kifo cha Kim: Mwanamke akamatwa Malaysia Mshukiwa wa mauaji ya Kim Jong nam akamatwa Mwili wa Kim Jong-nam walindwa vikali Mzozo waibuka kati ya Korea Kaskazini na Malaysia Mshukiwa wa mauaji ya Kim Jong-nam alilipwa $90 Hapo jana Ijumaa maafisa nchini Malaysia walisema, wana ushahidi wa kutosha, kumfungulia mashtaka Bw. Ri, na kwamba atarejeshwa kwao kwa kosa la kukiuka sheria ya uhamiaji ya nchi hiyo.

Aliyetangaza ''afya ya Mugabe imedhoofika'' akamatwa

Image
Waandishi wawili wa Zimbabwe wamekamatwa kuhusiana na ripoti ya gazeti moja ilioelezea kwamba afya ya rais wa taifa hilo Robert Mugabe 'imedhoofika' alipoelekea nchini Singapore kwa kile afisi ya rais huyo ilisema ni zaira ya kimatibabu. Muhariri wa gazeti la kibinafsi la NewsDay ,Wisdom Mudzungairi na mwandishi aliyeandika ripoti hiyo Richard Chidza hatahivyo wameachiliwa na ni sharti wajiwasilishe mahakamani. Wakili wao Obey Shava amesema kuwa wameshtakiwa kwa kuhujumu na kutusi afisi ya rais. Taarifa hiyo iliosema 'Mugabe yuko katika hali mbaya' ilinukuu duru zikisema kuwa rais huyo alisafirishwa kwa ndege siku ya Jumatano alfajiri. Mugabe: ''Naombewa nife'' Mugabe: ''Nilikufa kisha nikafufuka'' Mwanafunzi aliyempinga Mugabe akamatwa Mke wa Mugabe aamrishwa kurudisha nyumba tatu Mugabe alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya mwaka 93 na amekuwa katika mamlaka tangu 1980. Kulingana na chombo cha habari cha AP, wat...

Trump asema Obama alikuwa akidukua simu yake

Image
Rais wa Marekani Donald Trump amemshutumu mtangulizi wake kwa kudukua simu yake mwezi mmoja kabla ya kuchaguliwa kuliongoza taifa hilo. Rais Trump alichapisha ujumbe wa Twitter mapema siku ya Jumamosi akisema: Makosa sana! Nimegundua kwamba rais Obama alikuwa akidukua simu yangu katika afisi yangu iliopo Trump Tower kabla ya mimi kupata ushindi . Obama: Donald Trump ''hana ufahamu'' Obama asikitishwa na Trump Trump amlaumu Obama kwa maandamano Hawakupata kitu.Hii inaitwa McCarthyism!"{ kutumia njia mbaya kumchunguza mtu}. Aliongezea kwamba awali mahakama moja ilipinga uchunguzi...

Wapenzi wa jinsia moja katika soka watakiwa kujitokeza

Image
Image caption Chris Sutton asema ni wakati waenzi wa jinsia moja katika soka wanafaa kujitokeza Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa katika ligi ya Uingereza Chris Sutton amesema kuwa wakati umefika kwa wachezaji soka wanaounga mapenzi ya jinsia moja kujitangaza. Mwenyekiti wa shirikisho la soka nchini Uingereza Greg Clarke ameiambia kamati ya wabunge kwamba anahofia wachezaji watakabiliwa na matusi kutoka kwa mashabiki. Lakini Chris Sutton anasema kuwa matamshi ya Clarke yataonyesha kuwa soka haiko tayari kwa wachezaji wa mapenzi ya jinsia moja. ''Baada ya mchezaji wa kwanza wa mapenzi ya jinsia moja kujitangaza wengine watafuata'',alisema katika taarifa alioandika katika gazeti la Daily mail. Sutton mwenye umri wa miaka 43 aliongezea: hakuna muda mzuri kama sasa kwa wachezaji kujitangaza na kusema ''mimi ni mpenzi wa jinsia moja''. Wachezaji wengine watawaunga mkono.

Afcon 2017: Ivory Coast uso kwa uso na kocha wake wa zamani Herve Renard

Image
Image caption Morocco and Ivory Coast watachuana mara tatu ndani ya miezi michache ijayo Timu ya taifa ya Ivory Coast itapambana na kocha wake wa zamani Herve Renard baada ya kupangiwa katika kundi moja na Morocco katika michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika. Renard aliiongoza Ivory Coast katika fainali za kombe hilo mwaka 2015 na sasa anakwenda tena Gabon akiwa na kikosi cha nchi tofauti. Gabon watafungua mashindano hayo Januari 14, huku mchezo wa fainali ukipangwa kuwa Februari 5. Muonekano wa timu na makundi AFCON 2017 KUNDI  A Gabon Burkina Faso Cameroon Guinea Bissau KUNDI B Algeria Tunisia Senegal Zimbabwe KUNDI C Ivory Coast DR Kongo Morocco Togo GROUP D Ghana Mali Misri Uganda

Uefa: Barcelona yaiua Manchester City ya kocha wake wa zamani

Image
Image caption Messi amefunga magoli 10 katika michezo nane ya mwisho ya ligi ya mabingwa Ulaya Michuano ya klabu bingwa ulaya imeendelea kwa michezo nane kupigwa ambapo Arsenal waliiadhibu Ludogorets Razgrad ya Bulgaria 6-0, wakati Mesut Ozil akipata hat trick. Barcelona nayo wakiwa nyumbani walimdhalilisha kocha wao wa zamani Pep Guardiola kwa kumpa kichapo cha 4-0, Messi nae akipiga hat-trick, ambapo katika mchezo huo ilishuhudiwa mlinzi wa Man city Claudio Bravo akilambwa kadi nyekundu huku pia mlinzi wa Barcelona aliyeingia akitokea benchi Jeremy Mathieu naye akizawadiwa kadi nyekundu. Image caption Bravo atakosa mchezo wa maruduiano Novemba 1 Makosa ya wazi ya mlinzi wa Celtic Kolo Toure yakaipa Borussia Monchengladbach ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini, magoli yakifungwa na Lars Stindl pamoja na Andre Hahn. Image caption Wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi mnono Matokeo ya michezo mingine Bayern Munich 4-1 PSV Eindhoven Paris Saint-Germain 3-0 Basel Dynamo Kiev 0-2 Benfica...

Rooney akiri mambo ni magumu

Image
Image copyright REUTERS Image caption Rooney amepanga kustaafu soka ya kimataifa 2018 Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, amekiri kuwa sasa anakabiliwa na changamoto mpya katika Maisha yake ya Soka lakini amesisitiza bado hajaishiwa na ustadi wa kucheza. Rooney ambaye Jumatatu atatimiza miaka 31, alitoa kauli hiyo alipoongea na Waandishi wa habari siku chache baada ya Man United kutoka sare tasa 0-0 na Liverpool Jumatatu iliyopita huko Anfield huku yeye akianzia Benchi. Rooney ameuelezea mchezo dhidi ya Liverpool kuwa ilikuwa muhimu wasifungwe hasa kwa vile wanakabiliwa na mechi ngumu zijazo dhidi ya Fenerbahce Alhamisi jioni , Chelsea na Manchester City. Rooney, ambaye kwa sasa akiwa na Man United amechezea mechi 4 akitokea benchi, amesisitiza kuwa yeye yupo tayari wakati wowote akiitwa kucheza.

Pep Guardiola: Sitobadili filosofia ya mchezo wangu

Image
Image caption Mkufunzi wa Chelsea Pep Guardiola Meneja wa Manchester City Pepe Guardiola anasema kuwa hatobadili filisofia yake licha ya klabu yake kufungwa 4-0 na Barcelona katika uwanja wa Nou camp. Lionel Messi alifunga hat-trick dhidi ya Manchester City iliokuwa na safu ya ulinzi ilio legea huku kipa Claudio Bravo akipewa kadi nyekundu kwa kushika mpira nje ya eneo hatari.hakutakuwa na mabadiliko. ''Hadi siku ya mwisho ya kazi yangu kama mkufunzi nitajaribu kucheza kwa uwezo wetu'',alisema. Barcelona inaongoza kundi C na pointi tisa ,ikiwa mbele kwa pointi tano. City ilikuwa nyuma kwa bao moja katika dakika za kwanza za kipindi cha pili wakati Bravo aliposhika mpira na bahati mbaya ukamuangukia Luis Suarez.

Mvumbuzi wa nepi za kutupwa afariki dunia akiwa na miaka 94

Image
Image caption Valerie Hunter Gordon, katika picha mwaka jana, amefariki dunia kwake Beauly Valerie Hunter Gordon, mama wa watoo sita aliyevumbua nepi za kutumiwa na kutupwa ameaga dunia nyumbani kwake karibu na Inverness akiwa na umri wa miaka 94. Familia yake inasema alifariki October 16 huko Beauly. Aliovumbua nepi ya kwanza ya kutupwa iitwayo "Paddi" baada ya kumzaa mwanawe wa tatu Nigel, mnamo 1947 na baada ya kuchoshwa na kufua nepi za vitambaa. nepi hizo awali zilitengenezwa kwa nyloni, karatasi na pamba. Bi Hunter Gordon alitengeneza mamia ya nepi kwa kuzishona kwa cherehani jikoni kwake, na kuzisambaza kwa rafiki zake huku akizifanyia ukarabati mara kwa mara. Mumewe, Meja Pat Hunter Gordon, alilazimika kumsaidia kutengeneza nepi hizo aliporudi kutoka vitani Borneo. Nepi 'mbovu' Akizungumza na BBC mnamo 2015, Bi Hunter Gordon amesema laiona kazi kubwa kufua nepi na ndipo akaanza kutafuta atakazoweza kutumia na baadaye kuzitupa. "Nilidhani zauzwa - lakini z...

Popular This Month

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya