DIWANI WA CCM APOTEZA MAISHA KWA AJALI ASUBUHI YA LEO. | Darmpya
Diwani wa CCM katika kata ya Tindabuligi wilayani Meatu mkoani Simiyu, ndugu Seleman Mahega amepoteza maisha akiwa katika Hospitali ya Mwandoya alipokuwa akipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuapata ajali asubuhi ya leo.
Diwani huyo ni mmoja wa wale waliokuwa kwenye msafara wa mwenyekiti wa Uvccm Taifa Kheri James, uliopata ajali asubuhi ya leo mara baada ya magari katika msafara huo kugongana baada ya moja ya gari kwenye msafara kufunga breki ya ghafla iliyosababisha kutokea vumbi lilipelekea madereva katika magari ya nyuma yake kushindwa kuona vizuri.
Taarifa za msiba huo zimethibitishwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Antony Mtaka, ambaye ametoa pole kwa msiba huo na kuwaombea kupona haraka wale waliopata majeraha katika ajali hiyo.
Katika hatua nyingine Mtaka amesema jitihada za kuwapeleka katika Hospitali ya Rufaa Bugando, madiwani wengine wanne walioumia kwenye ajali zinaendelea.
from Dar Mpya Online TV
Comments