JOHN HECHE:WATU HAWAKO SALAMA NCHI HII, NI BAADA YA MDOGO WAKE KUUAWA NA POLISI | Darmpya
Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), mheshimiwa John Heche, amesema mdogo wake anayejulikana kwa majina ya Suguta Chacha, ameuuawa kwa kuchomwa kisu na polisi wa kituo cha Sirari usiku wa kuamka leo.
Mbunge huyo amedhibitisha kuuawa kwa ndugu yake huyo katika ujumbe wake kwenye ukarasa wake wa mtandao wa Twitter kuwa leo Aprili 27 2018 na kusema kuwa Suguta alichomwa kisu na polisi waliomkamata baada ya kumkuta baa akinywa pombe. Inadaiwa polisi wametekeleza tukio hilo huku akiwa na pingu mkononi.
“Watu hawako salama tena mikononi mwa polisi. Mdogo wangu Suguta amekamatwa na polisi jana usiku na ameuwawa na polisi kwa kuchomwa kisu. Najisikia maumivu mno, hii sio nchi ambayo tunaitaka. Najiuliza maswali mengi ni kwa vipi mtu amefungwa pingu anachomwa kisu tena na polisi.” Aliandika hivyo Mhe. Heche.
Aidha, Kamanda wa polisi mkoa Mara, RPC Mwibambe amethibitisha kutokea tukio hilo na wananchi wakazi wa Sirari wamezingira kituo hicho cha polisi baada kusikia kijana huyo ambaye inasemekana ana umri wa miaka 29 mkazi wa Sirari wilayani Tarime, kupoteza maisha akiwa mikononi mwa polisi.
from Dar Mpya Online TV
Comments