Mvumbuzi wa nepi za kutupwa afariki dunia akiwa na miaka 94

Valerie Hunter Gordon
Image captionValerie Hunter Gordon, katika picha mwaka jana, amefariki dunia kwake Beauly

Valerie Hunter Gordon, mama wa watoo sita aliyevumbua nepi za kutumiwa na kutupwa ameaga dunia nyumbani kwake karibu na Inverness akiwa na umri wa miaka 94.

Familia yake inasema alifariki October 16 huko Beauly.

Aliovumbua nepi ya kwanza ya kutupwa iitwayo "Paddi" baada ya kumzaa mwanawe wa tatu Nigel, mnamo 1947 na baada ya kuchoshwa na kufua nepi za vitambaa.

nepi hizo awali zilitengenezwa kwa nyloni, karatasi na pamba.

Bi Hunter Gordon alitengeneza mamia ya nepi kwa kuzishona kwa cherehani jikoni kwake, na kuzisambaza kwa rafiki zake huku akizifanyia ukarabati mara kwa mara.

Mumewe, Meja Pat Hunter Gordon, alilazimika kumsaidia kutengeneza nepi hizo aliporudi kutoka vitani Borneo.

Nepi 'mbovu'

Akizungumza na BBC mnamo 2015, Bi Hunter Gordon amesema laiona kazi kubwa kufua nepi na ndipo akaanza kutafuta atakazoweza kutumia na baadaye kuzitupa.

"Nilidhani zauzwa - lakini zilikuwa hazipatikani kokote," alisema.

"Ilishangaza sana kwamba haizjawahi kutengenezwa. Nilidhani itakuwa rahisi kwahivyo wacha nizitengeneze. Lakini haikuwa rahisi, ilikuwa vigumu kiasi .

"Kila aliyeziona alisema, Valerie, tafadhali nitengeneze na mimi moja? Kwahivyo niliishia kutengeneza kama nepi 600.

"Niliishia kwenye cherehani cha mamangu, kutengeneza nepi hizi mbovu."

Paddis zilitumika badala ya nepi za tauli ,ambazo ilikuwa ni lazima uzioshe baada ya matumizi.

"Kila mtu alitaka kuacha kusha nepi. Sikuhizi ni kama wanataka kurudi kuzifua tena - kila la kheri kwao," alisema Bi Hunter Gordon mwaka jana.

Paddi
Image captionTangazo kuhusu nepi za Paddi zilizovumbuliwa na Bi Hunter Gordon

Bi Hunter Gordon na mumewe walitia saini makubaliano na kampuni ya Robinsons mnamo 1948 kutengeneza nepi hizo 1949.

Miongoni mwa majina yaliofikiriwa kupewanepi hizo ni pamoja na Valette, Snappy, Napkins, Lavnets na Drypad. Jina Paddi lilichaguliwa baada ya mkutano kati ya Major Hunter Gordon na kundi la maafisa wakuu watendaji katika chuo cha uanajeshi Surrey, kwa mujibu wa mtandao wa Paddi.

Awali madaktari walikuwana shaka nazo nepi hizo, waliodhani zitawadhuru watoto.

Hatahivyo ripoti katika jarida la Lancet iliyoandikwa na daktari wa jeshi aliyemtumilia mwanawe Neppi hizo, ilisaidia kubadili mtazamo wa kitabibu na zikaanza kuuzwa katika maduka ya Boots.

PaddiImage copyrightHUNTER GORDON FAMILY
Image captionValerie Hunter Gordon na binti yake Frances katika tangazo la awali la Paddi

Zilitangazwa kama nepi zilizo nzuri na zilizoundwa na mama kwa ujuzi.

Kampuni hiyo ilifungwa katika miaka ya 1960, kufuatia kuzuka kwa Pampers kutoka Marekani.

Comments

Popular This Week

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

Popular This Month

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya