Posts

Showing posts with the label mpira

Afcon 2017: Ivory Coast uso kwa uso na kocha wake wa zamani Herve Renard

Image
Image caption Morocco and Ivory Coast watachuana mara tatu ndani ya miezi michache ijayo Timu ya taifa ya Ivory Coast itapambana na kocha wake wa zamani Herve Renard baada ya kupangiwa katika kundi moja na Morocco katika michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika. Renard aliiongoza Ivory Coast katika fainali za kombe hilo mwaka 2015 na sasa anakwenda tena Gabon akiwa na kikosi cha nchi tofauti. Gabon watafungua mashindano hayo Januari 14, huku mchezo wa fainali ukipangwa kuwa Februari 5. Muonekano wa timu na makundi AFCON 2017 KUNDI  A Gabon Burkina Faso Cameroon Guinea Bissau KUNDI B Algeria Tunisia Senegal Zimbabwe KUNDI C Ivory Coast DR Kongo Morocco Togo GROUP D Ghana Mali Misri Uganda

Rooney akiri mambo ni magumu

Image
Image copyright REUTERS Image caption Rooney amepanga kustaafu soka ya kimataifa 2018 Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, amekiri kuwa sasa anakabiliwa na changamoto mpya katika Maisha yake ya Soka lakini amesisitiza bado hajaishiwa na ustadi wa kucheza. Rooney ambaye Jumatatu atatimiza miaka 31, alitoa kauli hiyo alipoongea na Waandishi wa habari siku chache baada ya Man United kutoka sare tasa 0-0 na Liverpool Jumatatu iliyopita huko Anfield huku yeye akianzia Benchi. Rooney ameuelezea mchezo dhidi ya Liverpool kuwa ilikuwa muhimu wasifungwe hasa kwa vile wanakabiliwa na mechi ngumu zijazo dhidi ya Fenerbahce Alhamisi jioni , Chelsea na Manchester City. Rooney, ambaye kwa sasa akiwa na Man United amechezea mechi 4 akitokea benchi, amesisitiza kuwa yeye yupo tayari wakati wowote akiitwa kucheza.

FIFA: Argentina bado wababe, Tanzania washuka

Image
Image copyright AFP Image caption Argentina wameendelea kuongoza orodha hiyo ya ubora Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka duniani, ambapo vinara wamesalia kuwa Argentina. Wanafuatwa kwa karibu na mabingwa wa dunia Ujerumani, kisha Brazil wanashika nafasi ya tatu. Ubelgiji imeshuka nafasi mbili hadi nambari nne. Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi. Tanzania sasa inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka nafasi 12. Uganda wamo nambari 72 baada ya kushuka nafasi saba, Kenya wamepanda nafasi sita hadi nambari 85 nao Rwanda wamesalia nambari 107. Ethiopia wamo nafasi ya 126, Malawi 100 na Burundi 138. Nchi ya juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32. Orodha nyingine ya Ubora wa viwango itatolewa Novemba 24. Mataifa 10 bora duniani 1.Argentina 2.Ujerumani 3.Brazil 4.Ubelg...

Ubingwa Simba upo hapa

Image
Dar es Salaam.  Kimahesabu ni kama mlima mrefu, lakini kama rekodi ya msimu uliopita itafanya kazi, Simba ina mechi 12 muhimu, sawa na pointi 36 za kupigania ili  kuibuka na ushindi  na pengine kutwaa ubingwa msimu huu, ikimaliza ukame wa wake wa zaidi ya misimu mitatu. Timu hiyo iliyocheza mechi tisa hadi sasa,  huku ikiongoza ligi kwa pointi 23, inapaswa kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye 12 itakazocheza jijini Dar es Salaam, zikiwamo dhidi ya Yanga na Azam, ambako ndiko kuliifanya ikose ubingwa msimu uliopita. Msimu uliopita, Simba ilipoteza pointi 19 kwenye mechi ilizocheza Dar es Salaam wakati mikoani ilipoteza pointi tisa pekee. Iwapo Simba ingepata pointi kwenye mechi dhidi ya Toto Africans, Mwadui, Majimaji na Prisons na kisha kupata pointi nne tu kati ya 19 ilizopoteza nyumbani, ingefanikiwa kutwaa ubingwa. Pengine, pointi hizo ilizopoteza nyumbani (Dar es Salaam), zingeiwezesha (Simba) kutwaa ubingwa kwani ilimaliza ligi ikiwa na pointi 62 wakati mtani ...

Mchezaji wa Nigeria apigwa risasi na kufariki

Image
Image caption Mchezaji wa shooting Stars nchini Nigeria Izu Joseph kushoto Mwanasoka mmoja anayesakata dimba katika michuano ya ligi ya Nigeria, amepigwa risasi na kufariki nyumbani kwake katika jimbo la Bayelsa kusini mwa nchi hiyo. Mwaandishi wa BBC anasema kuwa Izu Joseph, beki wa timu ya Shooting Stars, aliuawa na askari waliokuwa wakikabiliana na wanamgambo katika eneo lenye utajiri wa mafuta. Miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa mapigano mapya katika eneo la Delta, huku wapiganaji wakitaka kupewa sehemu ya utajiri wa mafuta.

Ngassa afunga Goli lake la kwanza akicheza Fanja FC ya Oman

Image
MICHEZO Winga wa kimataifa wa  Tanzania anayecheza soka katika klabu ya  Fanja FC ya  Oman   Mrisho Ngassa   amefanikiwa kuanza maisha yake mapya ya soka katika klabu hiyo kwa kufunga goli akicheza mchezo wake wa kwanza toka ajiunge na klabu hiyo. Ngassa  ambaye amejiunga na  Fanja FC akiungana na aliyekuwa mshambuliaji wa Simba   Danny Lyanga  amefunga goli katika mchezo dhidi ya  Al-Nahda , mchezo ambao umemalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2.

RATIBA LIGI KUU YA UINGEREZA OCTOBA 2016

SAT 15 OCT Chelsea V Leicester 12:30 kick off Arsenal V Swansea 15:00 kick off Bournemouth V Hull 15:00 kick off Man City V Everton 15:00 kick off Stoke V Sunderland 15:00 kick off West Brom V Tottenham 15:00 kick off Crystal Palace V West Ham 17:30 kick off SUN 16 OCT Middlesbrough V Watford 13:30 kick off Southampton V Burnley 16:00 kick off MON 17 OCT Liverpool V Man Utd 20:00 kick off SAT 22 OCT Bournemouth V Tottenham 12:30 kick off Arsenal V Middlesbrough 15:00 kick off Burnley V Everton 15:00 kick off Hull V Stoke 15:00 kick off Leicester V Crystal Palace 15:00 kick off Swansea V Watford 15:00 kick off West Ham V Sunderland 15:00 kick off Liverpool V West Brom 17:30 kick off SUN 23 OCT Man City V Southampton 13:30 kick off Chelsea V Man Utd 16:00 kick off SAT 29 OCT Sunderland V Arsenal 12:30 kick off Man Utd V Burnley 15:00 kick off Middlesbrough V Bournemouth 15:00 kick off Tottenham V Leicester 15:00 kick off Watford V Hull 15:00 kick off West Brom V Man City 15:00 kick off C...

Popular This Month

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya