Ngassa afunga Goli lake la kwanza akicheza Fanja FC ya Oman
MICHEZO Winga wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka katika klabu ya Fanja FC ya Oman Mrisho Ngassa amefanikiwa kuanza maisha yake mapya ya soka katika klabu hiyo kwa kufunga goli akicheza mchezo wake wa kwanza toka ajiunge na klabu hiyo. Ngassa ambaye amejiunga na Fanja FC akiungana na aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Danny Lyanga amefunga goli katika mchezo dhidi ya Al-Nahda , mchezo ambao umemalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2.