Kwa nini nasita kujiunga na TEF – Fumbuka Ng'wanakilala | MICHUZI BLOG

Share



Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu TEF. Licha ya kasoro zake, pengine TEF kwa sasa ndiyo jumuiya ya waandishi wa habari Tanzania yenye umaarufu zaidi kuliko zote. Moja ya tuhuma kubwa dhidi ya TEF ni kuwa jukwaa hili limekuwa linatumika kama “kichaka” ambacho viongozi wa taasisi mbalimbali (hususan za umma) hujificha ili kujikinga na tuhuma za ufisadi.
TEF pia imekuwa inajulikana kwa kutoa matamko ya kufungia au kufungulia watu fulani wasiandikwe na vyombo vya habari nchini. Suala ambalo sisi wengine ambao siyo wanachama wa TEF tumekuwa tunahoji ni kuwa TEF ni jukwaa la wanachama (members only), hivyo basi, wanachama wa TEF wana *haki* ya kualikwa kwenye mikutano ya TEF na semina zinazoandaliwa na TEF na wana *wajibu* wa kupokea na kutekeleza maagizo ya TEF. Kwa muktadha huo huo, wahariri na waandishi ambao sio wanachama wa TEF hawana haki ya kuitwa kwenye vikao vya TEF, na hawana wajibu wa kutekeleza maagizo ya TEF.
Kumekuwa na dhana potofu kuwa maagizo na maamuzi yote ya TEF ni lazima yatekelezwe na waandishi wote wa habari, wahariri na taasisi zote za habari za Tanzania, hata wale wasio wanachama wa TEF bila kuzingatia dhana ya haki na wajibu.
Mara kadhaa tumesikia wahariri au vyombo vya habari vikiitwa wasaliti kwa kutotekeleza maagizo ya TEF bila kujali kama wahariri hao ni wanachama wa TEF au la. Je, ni nani amewapa TEF mamlaka ya kuwa wafanya maamuzi, watoa amri na wasemaji wa waandishi wa habari, wahariri na vyombo vyote vya habari vya Tanzania?

Lazima ieleweke wazi kuwa wenye wajibu wa kutekeleza maamuzi ya TEF ni wahariri ambao ni wanachama wa TEF tu. Wahariri ambao sio wanachama wa TEF hawana wajibu wowote ule wa kupokea maagizo ya TEF. Ni jukumu la TEF kuwashawishi wahariri hao waungane na msimamo wao kwa kujenga hoja.
Ni vyema TEF ikajitathmini na kurekebisha hii taswira mbaya iliyopo. Je, kuandaa semina ambazo wahariri wanalipwa posho na kufungia/kufungulia watu fulani wasiandikwe na vyombo vya habari ndiyo jukumu kubwa la TEF?
Ningependa kuona TEF ikijikita kukabiliana na matatizo ya msingi zaidi yafuatayo kwenye tasnia ya habari ya Tanzania:


1. Tatizo la rushwa kwenye tasnia ya habari ya Tanzania

2. Kuhakikisha kuwa baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania wanaacha kutoa maslahi duni kwa waandishi wa habari na kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa katika mazingira mazuri ya kazi

3. Kuondoa tatizo sugu la kuporomoka kwa maadili na weledi kwenye tasnia ya habari ya Tanzania

4. Kukemea na kukabiliana na kuongezeka kwa vitendo vya kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania

5. Kutoa dira kuhusu hatma ya vyombo vya habari nchini Tanzania kutokana na mazingira magumu ya biashara hiyo nchini kwa sasa

Pale ambapo TEF itakapojitathmini, naamini kwa dhati kuwa ina fursa kubwa ya kuwa jukwaa lenye nguvu na linaloheshimiwa na kuungwa mkono na waandishi wa habari na wananchi wengi zaidi nchini.

Naomba kuwasilisha.
Fumbuka Ng’wanakilala, 15 Agosti 2017

READ MORE

Share



from AutoMedia Tanzania
via Read More

Comments

Popular This Week

VIDEO | DJ Mwanga

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

KAMATI ZA BUNGE ZA HESABU ZA SERIKALI, NISHATI NA MADINI NA MIUNDOMBINU ZAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA. | sheila simba

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

ZIARA YA MHE MABULA MTAA KWA MTAA YAHAMISHIA OFISI ZA SERIKALI MTAANI KUTATUA KERO ZA WANANCHI. | Darmpya

MADHARA Ya Kuangalia Video za Ngono Na Namna Ya Kuacha | Udaku Special

SERIKALI YAZIONYA DINI KUJIHUSISHA NA SIASA | Darmpya

Popular This Month

VIDEO | DJ Mwanga

AUDIO | DJ Mwanga

KAMATI ZA BUNGE ZA HESABU ZA SERIKALI, NISHATI NA MADINI NA MIUNDOMBINU ZAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA. | sheila simba

ZIARA YA MHE MABULA MTAA KWA MTAA YAHAMISHIA OFISI ZA SERIKALI MTAANI KUTATUA KERO ZA WANANCHI. | Darmpya

SHILOLE KUTOKA NA KIGOLI | BONGO YETU

BREAKING NEWS: Tundu Lissu akamatwa | Emmanuel Shilatu

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya