Posts

MBALONI KWA KUMCHOMA MOTO MTOTO SABABU YA UDOKOZI | Darmpya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Eliza Denis (23) mkazi wa Makulu mkoani hapo kwa tuhuma za kumpiga sehemu mbalimbali za mwili na kumchoma moto mikononi mtoto wake wa kambo, Jackson Denis (5) kwa madai ya kudokoa chakula. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku jeshi la polisi likimshikilia mama huyo. “Huko maeneo ya Dodoma Makulu amekamatwa mama mmoja ajulikanae kwa jina la Eliza Denis ambaye ni mkulima na mkazi wa Dodoma Makuli kwa makosa ya kumpiga sehemu mbalimbali za mwili na… Source from Dar Mpya Online TV

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

Na Shabani Rapwi Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Saimon Msuva anaekipiga katika klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco usiku wa jana Jumamosi ametupia magoli mawili na kuifanya timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Ittihad Tanger katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Morocco (Botola Pro League). Msuva alifunga goli la kwanza dakika ya 2′ na dakika ya 30′. Ushindi huo wa magoli 2-0 unaifanya Difaa El Jadida kufikisha alama 24 wakiwa nafasi ya 9 huku Ittihad Tanger wakibaki nafasi ya 3 wakiwa na alama 27… Source from Dar Mpya Online TV

AZAM FC YAWATANGAZA MAKOCHA WAWILI, BAADA YA KUACHANA NA HANS | Darmpya

Na Shabani Rapwi. Uongozi wa klabu ya Azam FC jana Jumamosi, February 23, 2019 ulimetangaza rasmi kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Hans Van Der Pluijm baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili. Azam FC imefikia makubaliano ya kuachana na Hans pamoja na Msaidizi wake, Juma Mwambusi kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya hivi karibuni kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Katika mechi 5 za mwisho chini ya kocha Hans wamefungwa mechi 2 (Tanzania Prison 1-0 na Simba 3-1 ) na kutoa sare mechi 3… Source from Dar Mpya Online TV

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick L. Mpogolo amewataka viongozi wa Mkoa wa Dodoma na wana CCM kwa ujumla kushiriki katika vikao vya mashina na kuimarisha mashina wanayotokana nao ili kukiongezea mtaji Chama cha Mapinduzi. Ndg Mpogolo ameyasema hayo leo Wilaya ya Dodoma Mjini wakati wa maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa CCM kwa kuagiza Viongozi wote bila kujali nafasi zao kushiriki katika vikao vya mashina na kuwatambua mabalozi wao na kuwapa ushirikiano unaostahili kwa ustawi wa Chama. Akiwa katika ziara katika kiwanda cha Mvinyo cha CETAWICO ,Ndg Mpogolo… Source from Dar Mpya Online TV

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Waziri wa Nishati Mhe. Medard Kalemani kwenye ziara ya kikazi mkoani Mwanza iliyoanza hii leo akiwa wilayani Nyamagana amewasha mradi wa umeme Vijijini REA mtaa wa Nyakagwe katika Kata ya Buhongwa. Mhe. Kalemani amesema, serikali ya Mhe. John Pombe Magufuli imeongezewa KM 20 za ziada kutoka KM 25 zilizokuwepo awali Nyamagana katika mpango wa mradi wa umeme Vijinini REA na kufikia KM 45 ikiwa ni ombi maalum la Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ili kutatua changamoto ya umeme kwa wakazi walioko maeneo ya pembezoni. Akiongea na wananchi… Source from Dar Mpya Online TV

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWASHUKIA WAAJIRI WANAOKWEPA KODI KWA KUDANGANYA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI | Darmpya

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewashukia waajiri wote wanaotoa taarifa ambazo si sahihi za mishahara ya wafanyakazi kwa lengo la kukwepa kodi na pia kuchangia mchango mdogo katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii tofauti na mshahara wake. Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Anthony Mavunde wakati akiongea na waandishi wa habari katika Jiji la Mbeya na kubainisha kwamba Ofisi ya Kamishna wa Kazi inaendelea na ukaguzi wa kawaida ili kuwabaini waajiri hao na kuwachukulia hatua za… Source from Dar Mpya Online TV

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Zaidi ya tani 68 za Korosho zilizokuwa zimepimwa na wakulima katika vyama vya Msingi Chemana na China kata ya Chitekete Halmashauri ya wilaya Newala Mkoani Mtwara, zimerejeshwa kwa wakulima baada ya kukataliwa na Meneja wa maghala kuingizwa kwenye maghala makuu ya TANECU- Newala kwa kinachodaiwa kukosa ubora. Mwenyekiti wa chama cha Msingi Chemana Abilahi Ibadi, amesema Korosho zilizorejeshwa kwa wakulima ni tani 15.6 Kwa upande wake Mwenyekiti msaidizi wa chama cha Msingi China Juma Samli, amesema Korosho zilizorejeshwa kwa wakulima walio chini yake ni Tani 53… Source from Dar Mpya Online TV

Popular This Month

IGP SIRRO:NCHI YETU IKO SALAMA, NA TUNAO UWEZO WA KUFANYA UCHUNGUZI | Darmpya

TAWLA YATOA MAFUNZO YA JINSI YA KUSHUGHULIKIA WATOTO WALIO KATIKA UKINZANI NA SHERIA | VIJIMAMBO

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ELIBARIKI KINGU (CCM) AWEKA HISTORIA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo. | Mrisho’s Photography

“Ukipata mshtuko wa moyo, usipopata huduma ndani ya dk 90 ni kifo” – JKCI | Millardayo

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Popular All Time

MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA…WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI. | Darmpya

KOROSHO TANI 68 ZAREJESHWA KWA WAKULIMA KWA KUKOSA UBORA | Darmpya

MSUVA AWA MTAMU APIGA MBILI PEKE YAKE, DIFAA EL JADIDA | Darmpya

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO USIKU MMOJA | Darmpya

VIJIJI 20 MKOANI NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME UNAOFADHILIWA NA UJERUMANI | Darmpya

“SIJAONA SIMBA YA KUIFUNGA AZAM KESHO” – NGAONA | Darmpya

NYAMAGANA YAPATA KM 45 ZA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) | Darmpya

BABA NA MWANAE NA SHEMEJI MTU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA | Darmpya

MAFUNDI UMEME WATAKIWA KUWA NA LESENI YA EWURA KUPUNGUZA ‘VISHOKA’ NJOMBE | Darmpya