MWALIMU ASAKWA NA POLISI KILIMANJARO KWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa By Fina Lyimo na Bahati Chume, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz Hai . Polisi mkoani Kilimanjaro inamsaka mwalimu wa Shule ya Sekondari Lemira wilayani hapa anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne na kukimbilia kusikojulikana. Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa mzazi wa mwanafuzi huyo na mkuu wa shule wanashikiliwa ili kusaidia kupatikana kwa mawlimu huyo. Amesema mzazi aligundua kuwa mwanaye ana ujauzito wa miezi mitano na alipomuuliza alimwambia mhusika ni mwalimu wake. “Mzazi wa mtoto alimfuata mwalimu huyo aliyekubali kuwa ujauzito ni wake na kwamba atamuoa. Alimtaka aweke kwenye maandishi kuwa ujauzito ni wake na atamuoa,” alisema Mutafungwa. Amesema mwalimu huyo alikubali na kuandika kuwa atamuoa mwanafuzi atakapojifungua na kwamba, mkuu wa wilaya alipopata habari hizo alizifuatilia ili kujua sababu. Alisema alipoitwa kwa mkuu wa wilaya, mwalimu huyo a...